
Kiongozi huyo wa al-qaeda aliuwawa katika operesheni ya ardhini nje ya mji wa Islamabad kwa mujibu wa taarifa za kijasusi.
Bw Obama amasema baada ya ufyatulianaji wa risasi, majeshi ya Marekani ilichukua mwili wake. Bin Laden anashutumiwa kwa kuhusika katika baadhi ya vitendo vya ukatili ikiwemo mashambulizi mjini New York na Washington, mnamo Septemba 11, 2001.

Bw Obama anasema alielezea Agosti, mwaka uliopita, kuhusu kule Osama Bin Laden amejifisha. Kufuatia uchunguzi wa ujasusi waligundua amejificha mjini Pakistan

''Baada ya ufyatulianaji wa risasi, Bin Laden aliuwawa na mwili wale kuchukuliwa na majeshi ya Marekani'' rais Barack Obama amesema. Tayari vipimo vya DNA vimefanyika na kuthibitisha kuwa Osama ndiye aliyeuawa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.