ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, August 29, 2010

CHADEMA YAANZA RASMI KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU 2010. DR. SLAA ASEMA... "NITAFANYA MAAJABU NDANI YA SIKU 100 "

CHADEMA YAANZA KAMPENI KWA KISHINDO.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dr. Willbrod Slaa akizungumza leo jioni wakati wa uzinduzi wa kampeni na ilani ya chama chao mbele ya maelfu ya watu waliofika kuushuhudia uzinduzi huo katika viwanja vya jangwani. Dr Slaa alisema kuwa akipewa ridhaa ya kuiongoza nchi hii basi atahakikisha ndani ya siku 100 za kwanza,katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafanyiwa marekebisho makubwa na pia kuhakikisha mfumo wa Elimu hapa nchini unabadilishwa kabisa.

Sehemu ya umati wa wanachadema.

Mgombea Urais kwa Chama cha CHADEMA,Mh.Willibrod Slaa akiwapungia mkono wananchi mbalimbali waliofika kwenye viwanja vya Jangwani leo jioni mara ya kushuka kwenye gari.

Muasisi wa vyama vingi nchini na Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mabere Marando ambaye pia amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akionesha kitabu cha Ilani ya chama hicho mbele ya Wananchi waliofika katika viwanja vya jangwani leo.Marando aliongeza kwa kusema kuwa siku ya Jumatatu wataweka pingamizi kwa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mh Dr. Jakaya Kikwete kwa kudaiwa kukiuka baadhi ya sheria za Uchaguzi.


Aliyekuwa Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha CCM,na baadae akahamia chama cha CHADEMA hivi karibuni,John Shibuda akizungumza mbele ya wananchi leo jioni wakati chama hicho kilipokuwa kikizindua kampeni na Ilani yake katika viwanja vya Jangwani na kuhudhuriwa na mamia ya watu.

Maelfu ya wanachadema waliofika katika viwanja vya jangwani leo.
PICHA NA HABARI ZAIDI TEMBELEA:-www.michuzipost.com




ISHARA THABITI YA CHADEMA KATIKA VIDEO.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.