ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 3, 2012

WENJE MATATANI KWA LA KAIRO KISA HUNDI FEKI.


MBUNGE wa Jimbo la Rorya Bw. Lameck Airo “La-Kairo” amememshutumu Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Bw. Ezekial Wenje kwa kauli yake aliyoitoa hivi karibuni kwenye mkutano wa hadhara ambapo Wenje alidai kuwa alipewa hundi feki na Mbuge Lameck yenye thamani ya shilingi milioni tano (Tshs.5,000,000/=) ya benki ya Standard Charted kwenye harambee ya kuchangia madawati ya jimbo la Nyamagana jijini Mwanza.

Akizungumza ofisini kwake hii leo mbele ya vyombo mbalimbali vya habari Jijini Mwanza Bw. Airo amesema kuwa amesikitishwa kuona Mbunge huyo kijana kaanza kulewa madaraka ya uwakilishi na hata kudiliki kusema maneno ya uongo jukwani wakati akiwahutubia wananchi wa jimbo lake kwenye mikutano yake ya hadhara kwa nia ya kujiongezea umaarufu wa kisiasa.
Sikiliza alichosema kwa kubofya play..


Haya yanaibuka ikiwa ni takribani miezi sita sasa tangu kutolewa kwa cheki hiyo ambapo mbunge huyo wa Lorya anahoji kwamba kama Wenje anasema kuwa cheki hiyo ilibaunsi hivyo ni feki kwanini hakumtafuta kwa njia ya simu kuwasilisha malalamiko.

Mh. Lameck ameongezea kwa kudai kuwa hata siku fedha hizo zinatolewa alipigiwa simu na wadau wa benki kupewa taarifa za uhamishaji wa fedha.

 Alipotafutwa kwa njia ya simu ili kubaini ukweli wa haya yaliyosemwa na Bw.Airo,  Bw.Wenje  amekanusha kumtaja mbunge huyo kuwa alimpa hundi feki sambamba na kukanusha kiasi kinachotajwa kwamba kilitolewa kwamba si shilingi milioni tano bali ni milioni moja tu ambayo haikuwa na matatizo yoyote kwani Benki na aliweza kuitoa na kuhamishia katika Akaunti maalum kwa ajili ya kutengenezea madawati kama ilivyokuwa imekusudiwa.
Sikiliza kilichosemwa na wenje mkutanoni kwa kubofya play..


Mtandao huu uko mbioni kufuatilia stakabadhi za uhamishaji fedha hizo kubaini ukweli.


Katika hatua nyingine Bw.Airo ameendelea kusisitiza kauli aliyoitoa hivi karibuni kuwa hato gombea Ubunge wa Jimbo la Rorya baada ya kumalizika uongozi wake wa miaka mitano. 

Bw. Airo aliongeza kuwa CCM Wilaya ya Rorya ina wawakilishi wengi wazuri wa kuongoza na kusimamia ilani za Chama cha Mapinduzi, hivyo haoni sababu za kuhofia wanachama wenzake watakao jitokeza kugombea kuteuliwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha ugombea ubunge jimbo hilo naye atakuwa mstari wa mbele kupambana na kuhakikisha kuwa anampigia debe mgombea huyo hadi ushindi upatikane.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.