ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 17, 2016

MBUNGE WA JIMBO LA VUNJO,JAMES MBATIA AANDAA JIMBO LAKE KUKABILIANA NA MAJANGA.

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi taifa na Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akichokoza mada wakati wa kongamano la Elimu juu ya maafa katika jimbo hilo baada ya kukumbwa na mafuriko ,Kongamano lililofanyika katika shule maalum ya Viziwi na kuwashirikisha wenyeviti wa mitaa,Vijiji na Vitongoji,Maofisa watendaji,Madiwani,wakuu wa idara mbalimbali katika jimbo hilo.
Baaadhi ya washiriki wa kongamano hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akichangia mada katika kongamano hilo ambalo alikuwa mgeni rasmi pia,kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia na kulia Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila akichangia mada katika kongamano hilo lililotumika pia kuondoa itikadi za kisiasa huku akitoa wito kwa viongozi wote katika jimbo hilo kufanya kazi za maenedeleo bila ya kujali itikadi za kisiasa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji akichangia mada katika kongamano hilo lililoandaliwa na Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akielea namna ambavyo Wilaya hiyo ilivyopata athari kutokana na mvua zilizonyesha Aprily 24 na 25 mwaka huu.
Mwenyekiti wa mji mdogo wa Himbo ,Hussein Jamal akichangia mada katika kongamano hilo.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga,(kushoto) Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji (katikati) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila wakiteta jambo wakati kongamano hilo.
Baadhi wa wachangiaji katika kongamano hilo wakitoa michango yao.
Mbunge Mbatia akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Novatus Makunga.
Washiriki wa kongamano hilo wakiwa wamejigawa kulingana na kata wanazotoka ambazo zinafikia 16 katika jimbo la Vunjo wakijadili maafa yaliyozikumba kata hizo na namna ya kukabiliana nayo kabla ya mkutano huo kutoa maazimio.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Monday, May 16, 2016

RWANDA YAWATIMUA RAIA WA BURUNDI

Ripoti zinasema kuwa wale ambao walikataa kwenda kambi ya wakimbizi, walinyang'anywa mali zao na kisha wakafukuzwa.

CHANZO/BBC SWAHILI

Maafisa nchini Burundi wanasema kwamba Rwanda imewafukuza zaidi ya raia elfu moja mia tatu wa Burundi kutoka nchini humo katika kipindi cha wiki moja iliyopita, baada ya wao kukataa kuhamishiwa hadi katika kambi ya wakimbizi.

Afisa mmoja amesema kuwa wale ambao walikataa kwenda katika kambi ya wakimbizi, walinyanganywa mali yao na kisha wakafukuzwa.
Makumi kwa maelfu ya Warundi walikimbilia Rwanda tangu ghasia zilipoanza nchini mwao mwaka mmoja uliopita, kufuatia uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza wa kuwania Urais kwa muhula wa tatu kinyume na katiba.
Rwanda pia imewatimua Warundi ambao wameishi na kufanya kazi nchini humo kwa miaka mingi.

BUNGE MNATAKA KUTURUDISHA NYUMA - ZITTO KABWA

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) ameeleza Bungeni kusikitishwa na kitendo cha Bunge kutaka kuwafunga midomo wabunge waliotofautiana na kauli ya Waziri Nape Nnauye kuhusu Bunge kurushwa Live.

Akichangia hotuba ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Zitto amesema kwamba siku walipochangia kauli ya serikali kuhusu bunge kutorushwa live wabunge walio kataa kuunga mkono serikali wameitwa kuhojiwa.

''Mimi nashangaa sana siku Waziri Nape ametoa kauli ya serikali kuhusu kurushwa kwa matangazo ya Bunge wabunge tulichangia wapo waliounga mkono na wengine tukakataa kuunga mkono''- Amesema Zitto.

''Mheshimiwa Naibu Spika kiti chako kimetuita wabunge wote tuliopinga kauli ya Waziri Nape kwenye kamati ya maadili mimi jana nimepata barua kwamba mnatubana kusema mnazuia bunge lisionekane hata kutoa maoni ndani ya bunge mnatuita kwenda kuhojiwa, mnaturudisha nyuma namna hii? Amehoji Zitto.

Aidha Zitto ameonyesha pia kutoridhika na vyombo vya habari nchini runinga na redio kucheza nyimbo nyingi za wasanii wa nje n kusahau wasanii wa ndani na kuitaka serikali kupitia kwa waziri husika kuchukua hatua.

''Waziri Nape hili lipo kwako kama unataka kuwatetea wasanii hili wala halihiitaji kubadilisha sheria na kanuni za kontenti zipo chini ya waziri. Toa kanuni TCRA wazibariki kuwa asilimia 80 ya nyimbo zitakazopigwa kwenye redio na TV zetu ziwe za wasanii wetu wa Tanzania basi,” amesema Zitto.

MAYUNGA KUZINDUA VIDEO YAKE NA AKON KATIKA FINAL ZA Airtel Trace Music Stars

Mwanamuziki nguli wa miondoko ya R& B Akon akiwa na Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika  mwaka Jana.
Mayunga kuzindua video yake na Akon katika finali za Airtel Trace Music Stars

Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga anategemea kuzindua video yake  mpya ijulikanacho kama “Please don’t go away” aliyoifanya na mwanamuziki nguli duniani  Akon nchini Marekani

Nalimi Mayunga alipata nafasi  ya kurekodi wimbo huo  mara baada ya kuibuka kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika na kuwashinda washiriki wengi  kutoka  nchi 12 barani Afrika

Kibao hicho chenye mahadhari ya R& B  kimeanza kupigwa au kuchezwa leo katika radio mbalimbali nchini wakati ambapo video yake inategemewa kuzinduliwa rasmi siku ya Ijumaa 20 Mei 2016 wakati wa finali za msimu wa pili wa shindano la Airtel Trace Star 2016 linalowashirikisha washindi watano bora ambao wanashindania kitita cha shilingi milioni 50 ikiwa ni pamoja na nafasi kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya AfrikaAirtel Trace Star yatakayofanyika hivi karibuni nchini Nigeria

Akiongea kuhusu wimbo wake na Akon, Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga alisema “ kwa kweli namshukuru Mungu sana kwa kuniwezesha kufika mpaka hapa lakini pia nawashukuru Airtel kwa kunipa nafasi hii kubwa ya kuweza kurekodi wimbo na Mwanamuziki wa kimataifa Akon. Nafurahi sana sasa video hii iko tayari baada ya mashabiki wangu kuisubiri kwa muda mrefu. Natumaini nyimbo yangu itafanya vizuri ndani na nje ya nchi na kunipa fursa ya kuwa mwanamuziki nyota na hii ndio imekuwa ndoto yangu. Nawaomba watanzania waniunge mkono ili nyimbo zangu na muziki wangu uendelee kufanya vizuri.”

Aliongeza kwa kusema ”Napenda pia kuchukua nafasi hii kuwapongeza washiriki wa mwaka huu walioingia tano bora na kuwashauri waweke juhudi na nia ili waweze kujinyakulia ushindi na hatimae kutuwakilisha vyema katika mashindano ya Afrika na kurudi na ushindi nyumbani”. Aliongeza Mayunga

Naye Meneja uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando alisema , tunajivunia kuendelea kuwawezesha watanzania kuonyesha vipaji vyao ndani na nje ya nchi kupitia shindano hili la Airtel Trace Music Stars . Tunaamini video ya Mayunga itafanya vizuri  ikiwa watanzania tutamuunga mkono Star wetu huyu,  nachukua fursa hii  kuwaomba wadau mbalimbali wa tasnia ya muziki  kuisikiliza na kuipiga katika vyombo mbalilmbali kama radio, TV na klabu za muziki ili iwafikie mashabiki wengi”

Kufatia ushindi wake Nalimi Mayunga ameweza kupata mafunzo ya muziki toka kwa Akon pamoja na kurekodi kibao hicho kipya cha “Please don’t go away” na pia amepata nafasi ya kurekodi upya wimbo wake nchini South Afrika ujulikanao kama “Nice Couple”ambao unaendelea kufanya vizuri sana kwa sasa

SHUKURANI TOKA KWA FAMILIA YA ANKAL KUFUATIA MSIBA WA MWANAE MAGGID

Familia ya Ankal Muhidin Issa Michuzi  inapenda kutoa  shukrani nyingi sana sana kwa ndugu, jamaa, majirani, marafiki na wafanyakazi wenzie kwa kujitoa kwa hali na mali katika wakati huu mgumu wa msiba wa mawanae Maggid (pichani) aliyefariki huko Durban, Afrika Kusini Jumapili ya wiki iliyopita  na kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam juzi Jumamosi.
Ni vigumu mno kumshukuru mtu mmoja mmoja kutokana na wingi wenu na kwa jinsi kila mmoja wenu alivyojitoa na kuonesha upendo wa dhati kabla na baada ya mazishi. Tunaweza kujaza kurasa 200 kama hizi na tusiwe tumehitimisha robo tu ya shukrani zetu kwa kila mmoja wenu. Hivyo tunaomba radhi kwa yoyote ambaye hatutomtaja, kwani wafadhili wetu nyie mko wengi mno.
Pamoja  na hayo shukrani za kipekee ziwaendee Mheshimiwa Rais  Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mama Janeth Magufuli na familia yao yote, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt.  Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete na familia yao yote,  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na familia yake yote, Rais Mstafu wa awamu ya Tatu Mzee Benjamin William Mkapa na Mama Anna Mkapa na  familia yao yote, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Familia yake yote, Katibu Mkuu Kiongozi  Mhandisi Allan Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Ombeni Sefue  pamoja na wafanyakazi wenzie wote wa baba mfiwa kwa kuwa karibu naye katika wakati wote, na kuhakikisha kuwa  kila kitu katika msiba huu kinaenda sawasawa. TUNAWAOMBEA KWA MOLA AWAPE BARAKA ZAKE ZOTE...

Salamu zingine za kipekee ziwaendee watumishi  wote wa Ubalozi wetu Afrika kusini mjini Pretoria ambao wakiwa chini ya Brigedia Jenerali Kimaryo na Afisa wa Ubalozi kaka Awesi walisimamia maswala yote ya kuusafirisha mwili kutoka Durban kuja Dar es salaam. MOLA AWAONGEZEE PALE MTAPOPUNGUKIWA...

Vile vile shukrani za kipeke ziwaendee Viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Watanzania waishio Durban pamoja na Muslim Burial Society ya hapo hapo Durban ambao walihakikisha mwili wa marehemu unahifadhiwa, unakafiniwa na unasafirishwa kwa heshima zote.  ALLAH AWAJAALIE KATIKA KILA JAMBO...

Kwa Uongozi wa msikiti wa Maamur uliopo Upanga Dar es salaam pia familia inatoa shukurani  za kipekee kwa yote mliotutendea ikiwa ni pamoja na mwongozo wa kidini katika wakati wote wa msiba na mazishi.
Tutakuwa watovu wa fadhila endapo kama hatutatoa shukurani za kipekee kwa magrupu ya WhatsApp yote ambayo baba  mfiwa Ankal ni mwanachama. Shukurani hizi maalum ziwaendee Ma-Admin na wanachama wa Kariakoo Family Group (KFG), Dar es salaam Old Friends (DOF), Ma Best Group (MBG), Wanahabari, Tasnia ya Habari, Uongozi, Siasa na Matukio Mix, The New Team, TSJ Alumni, Zama Zile, The Brain Team, Jazz Fans, The Kop in Tanzania, LFC Bongo, Uswazi Academia, Tanzania Bloggers Network (TBN), The Legends Family, SID Tanzania Chapter, Mawasiliano, Team Michuzi, Amani Kwanza Group, Photojournalists TZ, PPAT Members, P Mamas, RUBY 15, Warembo wa KA, Mambachoz Group, Ndanshau Group, Empress Group kwa Fundi Mussa na wengi wengine wote katika Social media wakiongozwa na  Jamii Forum na VIJIMAMBO BLOG ya Marekani. TUMEHEMEWA MNO NA KUFARIJIKA SANA  KWA MICHANGO YENU YA HALI NA MALI. WE ARE HUMBLED. MBARIKIWE SANA, SANA, SANA...
Mwisho, lakini sio kwa umuhimu bali kwa nafasi na mpangilio, tunatoa shukrani za kipekee kwa shirikia la ndege la Emirates kwa kufanikisha usafiri wa mwili wa marehemu, hali kadhalika kampuni mahiri ya SWISSPORT kwa kusaidia logostics zote katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam.

HATUNA CHA KUWALIPA ZAIDI YA KUTOA SHUKURANI NA KUSEMA ASANTE SANA NA KUWAOMBEA KWA MOLA KILA MMOJA WENU AWABARIKI KATIKA SHUGHULI ZENU ZOTE...

Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un

AMIN!




Sunday, May 15, 2016

KUELEKEA JEMBEKA NA VODACOM HIVI NDIVYO 'VIPAJI FRESH' VILIVYOIBULIWA MWANZA.

Mmoja kati ya majaji wa mchakato wa kusaka vipaji Mwanza, wakuitwa  Mwaka Mzima kutoka Jembe Fm akitoa maksi zake kwa mmoja wa washiriki wa 'Vipaji Fresh' ambapo washiriki hao watakwenda kushindanishwa katika fainali itakayofanyika katika Tamasha la Jembeka Festival  uwanja wa CCM Kirumba jumamosi ya tarehe 21 Mei 2016.  Chini ya Udhamini wa Vodacom.
Hapa ilikuwa shughuli.
Maufundi katika 'VIPAJI FRESH'
Pia 'VIPAJI FRESH' ilisaka ma-Dj na hapa mmoja kati ya wakali akionyesha maujuzi yake kwenye mashine zilizofungwa Jembe Beach Mwanza.
Jimmy Kagaruki ni mtangazaji wa kipindi cha Mchakamchaka kupitia 93.7 Jembe Fm naye alishiriki kubaini 'VIPAJI FRESH' vilivyojitokeza Jembe BeachMwanza kuelekea Tamasha kubwa la Burudani la kila mwaka lijulikanalo kama JEMBEKA FESTIVAL linalidhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Nani aliibuka kuwa mkali zaidi yao ambaye atapanda jukwaa lile lile atakalopanda mwanamuziki mahiri kutoka nchini Marekani Neyo? Basi hapa Chief Judge wa 'VIPAJI FRESH' Deejay K-Flip alikuwa akitangaza washindi.
SwagZ nazo zilihusishwa.
'VIPAJI FRESH' Kupitia uchekeshaji ni Balaaaa.......
Majaji mezani.
Watu na watu  wao.
Dj katika 'VIPAJI FRESH'
Mwanza inavipaji ......imagine wote hawa  walikuwa wanasaka nafasi.
Si haba mmoja mmoja kupitia vipaji tofauti tofauti, iwe ni Dj, Mchekeshaji, Mtangazaji, Mkali katika kucheza au kipaji chochote kati ya hawa ataibuka kuwa mshindi katika 'VIPAJI FRESH' kwa tamasha kubwa la Burudani JEMBEKA FESTIVAL litakalo ungurumishwa uwanja wa CCM Kirumba jijini  Mwanza Jumamosi ya Tarehe 21 Mei 2016, chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.

MASHALI AMTWANGA MWARABU NA KUTWAA UBINGWA WA DUNIA

Bondia Francis Mashali (kulia) akimchapa konde mpinzani wake, Sajad Mehrabi wa Iran usiku wa Jumamosi Uwanja wa Ndani wa Taifa
Mashabiki wakiwa wamembeba Mashali baada ya pambano hilo
Refa Anthony Rutta akimuinua mkono Mashali kumtangaza mshindi wa pambano

Mgeni rasmi akimvalisha mkanda wa ubingwa wa dunia wa UBO Mashali baada ya ushindi wake
BONDIA Francis Mashali amefanikiwa kutwaa ubingwa wa dunia wa UBO uzito wa Super Middle baada ya kumshinda kwa pointi Sajad Mehrabi wa Iran usiku wa Jumamosi Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.

Mashali anayekwenda kwa jina la utani la Simba, alipewa ushindi huo na majaji wote watatu katika pambano hilo kali na la kusisimua liliodumu kwa raundi 12.

Mehrabi alionekana ni bondia bora zaidi ulingoni, lakini staili ya kupigana kwa kutafuta ushindi wa Knockout (KO) ilimponza kupoteza pambano hilo kwa pointi.

Mashali alilianza vizuri pambano hilo akipigana kwa tahadhari na kukwepa kabisa mtego wa kupigwa kwa KO na mpinzani mwenye ngumi nzito kutoka bara Asia.

Akiongozwa na bondia nyota wa zamani nchini, Rashid Matumla, Mashali alionekana kupigana kwa utulivu, umakini na kujiamini jambo ambalo liliwafanya mamia waliojitokeza kushuhudia mchezo huo kumshangilia tangu mwanzo.

Baada ya raundi saba, Mehrabi alionekana kama kuanza kuchoka na kasi yake kupungua na Mashali akafanya vizuri zaidi katika raundi ya saba hadi ya tisa.

Hata hivyo, katika raundi ya 10, Mehrabi alirudi na kasi mpya na kufanikiwa kumtandika makonde mazito mfululizo Mashali alIyepepesuka hadi kwenye kamba.

Mashali alirejea mchezoni baada ya refa Anthony Rutta kusimamisha pambano kwa muda kumsikilizia, lakini hakuweza kumalizia vizuri raundi hiyo,

Katika raundi ya 11, Mehrabi aliingia na moto tena, lakini safari hiyo Mashali alirudi kwa tahadhari na kufanikiwa kumpunguza kasi mpinzani wake huyo.

Raundi ya 12 mabondia wote walipigana sawa ingawa kwa ujumla ngumi za Mehrabi zilionekana kuwa nzito kuliko za Mashali.

Mehrabi hakuwa na malalamiko baada ya pambano zaidi ya kumkumbatia mpinzani wake na kumpongeza kwa ushindi huo.

Katika mapambano ya utangulizi, bondia mwingine nyota wa Tanzania, Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ alimshinda Ben Sajjabi wa Uganda kwa KO raundi ya pili pambano la uzito wa Super Bantam.
Mtanzania mwingine, Nassib Ramadhani alimshinda kwa pointi Reemy Iga wa Uganda pia pambano la uzito wa Super Bantam.

Allan Kamote wa Tanzania alitoka sare na Salim Chazama wa Malawi katika pambano la uzito wa Light raundi sita.

Ramadhani Shauri wa Tanzania alimshinda kwa pointi Osgood Kayuni wa Malawi pambano la uzito wa Welter raundi sita.

Saleh Mkalekwa alitwaa taji la UBO uzito wa Welter baada ya kumshinda James Onyango wa Kenya kwa pointi pambano la raundi 10, wakati Twaha Kiduku alimshinda kwa KO raundi ya kwanza Fred Nyakesa wa Kenya pambano la uzito wa Light Heavy raundi sita lisilo la ubingwa.

Bondia wa kike, Lulu Kayage alitoshana nguvu na Chiedza Hamakoma wa Malawi katika pambano la raundi nne uzito wa Welter na Dickson Mwakisopile alimshinda kwa pointi Mtanzania mwenzake, Ramadhani Ally katika pambano la uzito wa juu raundi nne.

Shaaban Kaoneka alimshinda Mtanzania mwenzake, Hassan Mwakinyo kwa KO raundi ya tano, wakati Issa Nampepeche hakutokea kupigana na Baina Mazola katika pambano la uzito wa Super Feather raundi sita.  

TAANESCO MKOA WA PWANI YAMAKAMATA MMILIKI WA YADI YA MAGARI KWA WIZI WA UMEME

NA MWANDISHI WETU

SHIRIKA la ugavi wa umeme Tanesco Mkoa wa Pwani limefanikiwa kumkamata moja ya mteja wake  ambaye ni  mmiliki wa yadi ya magari ya White star iliyopo kiluvya kwa Komba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kwa kosa la kuhujumu miundombini kwa kufanya wizi baada ya kuamua   kujiunganishia umeme  kinyemela  wa njia tatu kinyume na taratibu na sheria za nchi.

Mteja huyo alikamata baada ya kufanyika kwa msako  mkali kwa wateja ambao wanaiba umeme na kuweza kubaini katika yadi hiyo kuna hujuma ambayo imefanyika ya kujiunganishia umeme bila ya kufuata taratibu zozote za Tanesco.

Akizungumza katika eneo hilo la tukio Afisa Usalama wa Tanesco Mkoa wa Pwani Henry Byarugaba alisema kwamba baada ya kufanya ukaguzi waliweza kukuta mtaja huyo alijulikana  kwa jina la Munila Mbowe ambapo aliweza kukamatwa na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Kibaha.


Byarugaba alisema kwamba mteja huyo alikuwa anatumia umeme wa wizi kutokana na kujiunganishia laini tatu za nyaya ambapo kutokana na wizi huo ameseza kulisababishia hasara shirika zaidi ya shilingi milioni 50.

“Kama mnavyoona ndugu waandishi katika kufanya msako wetu wa kawaida tumeweza kumkamata mmiliki wa yadi ya magari ya white star ambayo ipo kiluvya kwa kombo kwa kosa la kuiba umemembila ya kuzingatia sheria zozote na kwamba ameweza kujiunganishia njia tatu ambazo zilikuwa zinapitisha umeme kwa matumizi ambayo sio sahihi katika eneo hilo,”alisema Byarugaba.

Aidha Byarugaba alisema mteja huyo amekuwa akifanya vitendo vya kuhujumu miundombinu yao na kufanya uharibufu mkubwa hali ambayo inaweza kuleta madhara makubwa ya kutokea kwa majanga ya moto kutokana na kujiunganishia umeme  bila ya kuwatumia wafanyakazi wa shirikika la umemem Tanesco.

Pia alisema kuwa mteja huyo amekuwa ni sugu kwa kipindi cha muda mrefu kutokana na kujirudia kwa makosa kama hayo kwani mwaka jana wakati wanafanya msako kwa wateja wao wanaohujumu miundombinu waliweza kumkuta akiiba tena  umeme na walimpeleka polisi na hatua kali za kisheria ikiwemo kumlipisha faini.

“Jamani ndugu waandishi huyo mteja wetu ambaye anajulikana kwa jina la Munira Mbowe amekuwa akifanya matukio haya kwa kipindi cha muda mrefu na kutokana na hali hii amelitia hasara shirika la umeme, maana mwaka jana tulimkamata tena akiifanya vitendo kama hivi na tulimfukisha katika vyombo vya sheria lakini nashangaa amekuja na staili hyingine ya wizi kwa kutumi tena njia tatu  za umeme hii ni hatari sana.

Kwa upande wake mmoja ya wamilii ya yadi hiyo ya Munira Mbowe alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusina na tumuma za wizi huo alisema kwamba yeye afahamu lolote juu ya suala hilo kwani mara nyingi yeye  anafanyia shughuli zake jijini Dar es Salaam.

“Ni kweli tumekutwa na kosa na kuiba umeme lakini jamani waandishi  nataka niwaeleze kuwa mimi siusiki na kingine nawaomba msinitoe katika vyombo vya habari kwani haya ni maisha tu, sio vizuri kunitoa jamani mimi sihusiki kabisa katika wizi huu labda anaweza kuwa ni mlinzi amefanya hivyo au mume  wangu amenificha maana wanaume ni wasiri sana,”alijitetea Munira.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Taneso Mkoa wa Pwani Selemani Mgwila alisema kwamba kitendo alichokifanya mteja wao ni kosa kubwa sana kwani umeme waliokuwa wanatumia katika yadi hiyo ulikuwa unapotea bure na kusababisha upotevu mkubwa wa mapato.


Aidha Mgwila aliwaomba wananchi wote wa Mkoa wa Pwani kuepukana na watu ambao wanajifanya ni watumishi halali wa tanesco na endapo wakiwabaini wahakikishe wanatoa taarifa mapema kwa vyombo vya dola ili waweze kuchukuiliwa hatua kali za kesheria kwani baadhi yao ni matapeli.

SHIRIKA la umeme Tanesco Mkoa wa Pwani limekuwa likiingia hasara kubwa kutokana na baadhi ya wateja wake kuamua kujiunganishia umeme kinyemela pasipo kuzingatia sheria na taratibu na wakati mwingine kupelekea kutokea kwa majanga ya moto.

MAGAZETI YA LEO> MAALIM SEIF AMTISHA SHEIN. MAGUFULI AIVUTIA MARAKANI. UINGEREZA KUISAIDIA TANZANIA. MAJALIWA AFICHUA SIRI.


CH10: Marekani, Uingereza zakoshwa na Magufuli, Wakwepa kodi kitanzini, Maalim Seif amtisha Dr.Shein, Malawi yakamata boti ya Tanzania. Fuatilia Uchambuzi wa Magazeti 



TBC: Maalim Seif amtisha Shein, Magufuli aivutia Marekani, Uingereza kuisaidia Tanzania, Majaliwa afichua siri. Peruzi Magazeti ya leo.

MAZISHI YA MTOTO WA UNCLE MICHUZI.

Mwili wa marehemu ukiingizwa katika msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es salaam leo tayari kwa kuswaliwa kabla ya mazishi.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete (kushoto) akimfariji  baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi. 
Mama wa marehemu (aliyevaa nguo nyeupe) akiwa na ndugu wa karibu wakiomboleza. 
Baba wa marehemu akiwa na viongozi wa dini wakiombea mwili wa marehemu dua.
Mke wa Rais mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na ndugu wa marehemu. 
Baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi akipata chakula.
Mke wa Rais mama Janeth Magufuli (kulia) akiwasili msibani Wazo hill akiwa  na baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi.
Baba wa marehemu akiwa na Balozi Cisco Mtiro na baadhi ya waombolezaji.
Baba wa marehemu (mwenye kofia), Ankal Issa Michuzi akipewa pole na baadhi ya waombolezaji mara baada ya maziko ya mtoto wake Maggid Muhidin Michuzi (18)yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akimpa pole Issa Michuzi.
Rais Mstaa mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete akimfariji Ankal Issa Michuzi.
Issa Michuzi (mwenye kofia) akifuatiwa na Rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,  kulia kwake ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe Ombeni Sefue. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi  John Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo wakati maziko.
Waumini wakiomba dua.
Baba wa marehemu Issa Michuzi (katikati) akiwa na huzuni akiwa na Rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,  kulia kwake ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde 
Baba mkubwa wa marehemu, Ismail Issa Michuzi akitoa shukrani kwa walioshiriki mazishi ya mtoto wao.
Mroki Mroki ambaye aliyekuwa MC akitoa ya muongozo wakati wa mazishi.
Waombolezaji wakiweka udongo kwenye kaburi la marehemu.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi akiweka udongo.
Waziri Mkuu mstaafu Jaji  Joseph Sinde Warioba akiweka udongo kaburini.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiweka udongo kaburini.
Baba wa marehemu Ankal  Issa Michuzi akiweka udongo kaburini.
Mwili wa marehemu ukiwekwa kaburini.
Mwili ukiwasili makaburini.

Rais mstaafu Jakaya Kikwete akimpa pole baba wa marehemu, Ankal  Issa Michuzi. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi  John Kijazi. Picha zote na Francis Dande