Na Fredy Mgunda, Iringa.
Wananchi wa Kijiji
cha Mgera kata ya Kiwele wilaya ya Iringa wamemlalamikia mwenyekiti wa Kijiji
hicho kwa kuwapora ardhi ya wananchi kwa kutumia mabavu na madaraka aliyonayo
ya kiungozi.
Akizungumza kwenye
mkutano wa mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo wa kupokea malalamiko
ya wananchi, wananchi hao walisema kuwa mwenyekiti huyo amekuwa akiwanyanyasa
na kuongeza serikali ya Kijiji kwa mabavu.
Ayubu Mtweve ni
mwananchi wa Kijiji hicho alisema kuwa mwenyekiti wa Kijiji Lucas Mgata
amempora ardhi yenye zaidi ya hekari mbili ambazo anamiliki kwa zaidi ya miaka
thelathini(30) jambo ambalo linawashangaza wengi.
Mtweve alisema kuwa
mwenyekiti huyo amekuwa anajihusisha kwenye migogoro ya ardhi kwa kupora ardhi
za wananchi kwa asilimia kubwa kutokana na kutumia madaraka vibaya aliyonayo.
Alisema kuwa
amelalamika kila kona lakini hakuna kiongozi yeyote aliyefanikiwa kutatua
mgogoro huo jambo ambalo lilimfanya yeye na wenzake kuandamana hadi ofisi ya
mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ili awasaidie kutatua mgogoro huo
wa ardhi baina ya wananchi na mwenyekiti huyo.
Mtweve alisema kuwa
mwenyekiti huyo anatumia mabavu kupora ardhi za wananchi Jambo ambalo
linawafanya wananchi wa Kijiji cha Mgera kukosa amani ya kuishi na kumiliki
ardhi.
"Yaani anapora
ardhi halafu ukianza kufuatilia anatishia kukuuwa na kukuweka ndani jambo
wananchi wengi wamekuwa waoga kufuatilia haki zao hivyo nilipoanza kufutilia
bila uoga ndipo wananchi wengine wanajitokeza kulalamika hadi kufika kwa mkuu
wa wilaya"alisema Mtweve.
Veronica Chusi ni
bibi mwenye umri wa miaka 84 anamlalamikia mwenyekiti wa Kijiji hicho Lucas
Mgata kwa kupora ardhi yake kwa njia ya kuazima ardhi aitumie kwa kilimo lakini
baadae akaifanya ikawa ya kwake jambo ambalo anasema kuwa kupora ardhi kwa
kutumia mabavu.
Chusi alisema kuwa
ameanza kuitumia ardhi hiyo kabla ya mwenyekiti huyo hajazaliwa iweje leo anasema
ya kwake na ameridhishwa na wazazi wake Jambo ambalo sio la kweli hivyo toka
ameingia madarakani kiongozi huyo amekuwa na tabia ya kupora ardhi kwa
Wananchi.
Bibi huyo alienda
mbalimbali zaidi na kusema ukilalamika anakutishia kukuua jambo ambalo
linawafanya wananchi wengi kuacha kufuatilia haki zao.
"Mwenyekiti
anwike ardhi yetu kwakutumila nguvu,pe mwana mdodo atufile bahaa akutuanuka
ilieneo letu iserikali twisuka mtange tuvayenu tufayenu tunamiaka zaidi ya
themanini tugapakuliwa tutegemee bahaa", alisikika Mzee huyo
akiongea kwa lugha ya kihehe na kiswahili kuomba msaada wa kusaidia kutatua
mgogoro huo.
Bibi Chusi alimazia
kwa kusema kuwa ukifika Kijiji hapo ukimuuliza kila wananchi atakuambia kuhusu
uporaji wa ardhi anaoufanya mwenyekiti huyo wa Kijiji kwa kuwa sio kificho
Tena.
Naye bibi Lusia
Mbugano mwenye umri wa miaka 90 alisema kuwa mwenyekiti huyo amekuwa
akiwanyanya ardhi Mara kwa mara na walikuwa wanakaa kimya kutokana na kutishiwa
amani na kiongozi huyo.
Bibi Mbugano alisema kuwa
mara ya kwanza aliwapora ardhi ambayo waliachiwa urithi na marehemu baba yai
Mzee Mwesimpya Nyaulingo miaka ya 1937 huko lakini kiongozi huyo amekuwa
akitumia njia mbalimbali ikiwemo kuwatishia kupora ardhi.
Alisema kuwa hivi
sasa hana hata eneo la kulima kutokana na kupora maeneo yote na mwenyekiti huyo
wa Kijiji cha Mgera hivyo ameiomba serikali kusaidia kutatua mgogoro huo.
Bibi Mbugano alisema
kuwa hivi karibu mwenyekiti huyo amempora tena ardhi ya hekari tatu ambazo
alikuwa amebakiwa nazo hivyo unakaribia wakati wa kilimo na hana eneo la kulima
anaiomba serikali kuharakisha kutatua mgogoro huo.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa Kijiji cha Mgera Lucas Mgata alisema kuwa tuhuma zote alizopewa
na wananchi sio za kweli na wanamsingizia tu kutokana na utendaji wake wa kazi.
Mohamed Hassan Moyo ni mkuu wa
wilaya ya Iringa alilazimika kufika katika eneo lenye mgogoro huo wa ardhi na
kubaini kuwa kunamgogoro ambao unatakiwa kutatuliwa haraka.
Moyo alisema kuwa
atatuma wataalam kuchunguza malalamiko ya wananchi wa kijiji cha Mgera wanaodai
kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji chao amekuwa chanzo cha migogoro kwa
kupora maeneo ya ardhi ya Wananchi
Alitoa kauli
hiyo baada ya wananchi kudai kuwa mwenyekiti wao amezusha hofu katika kijiji
hicho baada ya kujimilikisha ardhi isivyo halali maeneo yenye makazi ya watu
pamoja na mashamba.
Moyo aliyefika katika maeneo yenye mgogoro amebaini kuwa walalamikaji pamoja na mlalamikiwa , wote hawana hati za umiliki wa ardhi hiyo hivyo amepiga marufuku kufanyika kwa shughuli zozote hadi ufumbuzi utakapopatikana.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.