Mratibu wa Dawati la Michezo Idara ya Utawala wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Salome Mziray kulia akipokea jezi kutoka kwa benki ya NMB kwa ajili ya Mashindano hayo
Na Oscar Assenga,TANGA.
TIMU ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imetamba kufanya vizuri katika Michuano ya Shimiwi inayoendelea Jijini Tanga ili kuweza kunyakua Ubingwa wa Jumla.
Tambo hizo zilitolewa leo na Meneja wa timu hiyo Moshi Saidi wakati akizungumza na mtandao huu ambapo alisema hilo linatokana na maandalizi kabambe waliyoyafanya kuelekea michezo hiyo.
Moshi alisema kwamba kutokana na umahiri ulionao timu zao za mpira wa miguu,pete,na kamba ikiwemo michezo mengine wana matumaini makubwa ya kuipa kipigo kila timu itakayokutana nayo.
"Labda niwaambie kwamba sisi tumekuja Tanga kushriki Mashindano ya Shimiwi kwa lengo la kutafuta ushindi na tuweze kurudi na vikombe vya kutosha na sio vyenginevyo kama waamuzi watafuata sheria na kanuni kwani wachezaji wetu wana hari ya ushindi tu"Alisema Meneja huyo.
Awali akizungumza wakati wa mashindano hayo Mratibu wa Dawati la Michezo Idara ya Utawala wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Salome Mziray alisema ushindi wa watmuishi wa umma katiika michezo ina faida nyingi ikiwemo kuongeza tija na ufanisi kazini.
Salome alisema pia kuna umuhimu wa Shimiwi kuhakikisha waendelea kuzingatia ratiba vema ikiwemo kuondokana na mamluki kwani wanaotakiwa kuchgeza lazima wawe watumishi wa umma na sio vyenginevyo.
"Lakini pia waendelee kuboresha na kuzingatia masuala muhimu yanayoekelezwa kwenye mashindano hayo kama timu inatakiwa kufika saa moja mchezo wake usisogezwe mbele sana kwa sababu watumishi tunashriki michezo mbalimbali hivyo ni bora wajali muda wa kuanza mchezo mmoja hadi mwengine"Alisema
Mashindano hayo yalifunguliwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.