ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 5, 2022

MHUDUMU MWINGINE WA AFYA AANGUSHWA NA EBOLA -UGANDA


Wizara ya Afya nchini Uganda imethibitisha kifo cha mhudumu mwingine wa afya, ambaye aliaga dunia usiku wa kuamkia Jumatano, Oktoba 5. Mgonjwa huyo alifariki baada ya kuugua ugonjwa wa Ebola kwa siku 17. 

 Waziri wa Afya Jane Ruth Aceng, alisema mgonjwa huyo mwenye umri wa miaka 58, alifariki katika Hospitali ya Fort Portal (JMedic) baada ya kuugua ugonjwa huo kwa siku 17. 

Marehemu ni mhudumu wa afya wa nne kufariki kutokana na ugonjwa wa Ebola.

 "Mgonjwa huyo mwenye umri wa miaka 58, aliaga dunia saa 4.33 asubuhi katika Hospitali ya Fort Portal (JMedic) baada ya kuugua ugonjwa huo kwa siku 17," Aceng alisema kupitia taarifa kwenye ukurasa wake wa Twitter. 

 Wahudumu wa afya nchini humo walipata virusi hivyo walipokuwa wakimtibu mgonjwa wa kwanza aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa huo. 

Kifo chake ni kufuatia kingine cha mwanafunzi wa utabibu Mtanzania, ambaye alikuwa sehemu ya timu hiyo na alifariki dunia mwishoni mwa juma lililopita Wahudumu wa afya walikuwa wamegoma wakizua wasiwasi wao ya kutokuwa na vifaa vya kutosha kujilinda katika siku za kwanza za mlipuko wa ugonjwa huo. 

Kufikia sasa, visa 43 vya virusi hivyo vimethibitishwa huku kumi kati yao wakifariki. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.