Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto) akitazama mtambo wa kusaga Madini ya Jasi na kisha unga wake (gypsum powder) hutumika kutengeneza Chaki katika kiwanda cha Dobercolor kilichopo katika Kijiji cha Majengo, Itigi.
Eneo la kuchomea Madini ya Jasi kabla hayajasagwa na kuwa unga (Gypsum powder) katika Kiwanda cha Kusaga Mawe ya Jasi cha RSR kinachomilikiwa na Mtanzania, Rashid Rashid kilichopo katika Kijiji cha Sanjaranda, Itigi.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kushoto) akitazama hatua ya uchomaji wa Madini ya Jasi kwenye kiwanda cha kampuni ya mzawa cha RSR kinachomilikiwa na Rashid Rashid (kushoto) kilichopo katika Kijiji cha Sanjaranda, Itigi kabla ya kusagwa kuwa unga (Gypsum powder) na baadaye kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa ajili ya kuuzwa.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (aliyesimama) akizungumza na Wafanyakazi, Wachimbaji na Wafanyabiashara wa Madini ya Jasi (hawapo pichani) wakati wa ziara yake Itigi Mkoani Singida. Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Pius Luhende.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Machimbo ya Jasi, Wachimbaji na Wafanyabiashara wa Madini ya Jasi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) wakati wa ziara yake Itigi Mkoani Singida.
WALIOSHINDWA
KUCHIMBA JASI KUFUTIWA LESENI
Serikali imesema Wachimbaji wa Madini ya Jasi walioshindwa kuendeleza
maeneo yao sheria itachukua mkondo wake ikiwemo kufutiwa leseni zao na maeneo
yao kumilikishwa Wachimbaji wengine wenye nia ya kufanya uchimbaji.
Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alisema hayo Desemba 11, 2017 wakati wa
ziara yake kwenye machimbo ya Jasi Wilayani Manyoni, Mkoani Singida.
Nyongo
alitoa kauli hiyo kufuatia malalamiko ya baadhi ya wachimbaji wa madini hayo ya
kukosa maeneo ya kutosha kufanya shughuli za uchimbaji husika na huku maeneo
mengi yakiwa chini ya umiliki wa watu wasioyaendeleza.
Alisema
leseni zilitolewa ili uchimbaji ufanyike na kwakua waliopewa leseni wameshindwa
kuendeleza maeneo husika, sheria itachukua mkondo wake ikiwemo kuwaandikia hati
ya makosa (default notice) na endapo watashindwa kutekeleza maelekezo watakayopewa,
leseni za uchimbaji wa madini husika zitafutwa na maeneo yao kumilikishwa
wengine.
Alimuagiza
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati, Singida, Sosthenes Massola
kufuatilia suala hilo ili hatua stahiki zichukuliwe mapema iwezekanavyo.
Vilevile, Naibu
Waziri Nyongo alitoa onyo kwa wachimbaji wanaoshindwa kulipa fidia ya umiliki
wa ardhi kwenye maeneo yaliyokuwa yanamilikiwa na watu wengine wakiwemo
wakulima.
Alitoa
onyo hilo kufuatia malalamiko kutoka kwa wananchi ambao walisema baadhi ya
wachimbaji wa Madini ya Jasi walianza kufanya shughuli zao za uchimbaji bila ya
kukubaliana na wenyeji waliowakuta kwenye maeneo hayo jambo ambalo walisema
limewaletea usumbufu na kuwarudisha nyuma kimaendeleo.
"Sisi
wakulima tunanyasika, mchimbaji anakuja na kuanza kuchimba bila makubaliano
yoyote," alisema Hamis Said ambaye aliwatuhumu wachimbaji kuvamia eneo
lake bila ridhaa yake.
Naye
Hamisa Rashid ambaye alijitambulisha kuwa ni mkulima alishauri kwamba
wachimbaji kabla hawajaanza shughuli zao wawatafutie maeneo mbadala ili
wakaendeleze shughuli zao za kilimo.
Naibu
Waziri Nyongo alisema haiwezekani mchimbaji apewe leseni hali ya kuwa hana
uwezo wa kulipa fidia kwa wananchi ambao amewakuta katika eneo analotaraji
kufanya shughuli za uchimbaji.
"Hii
ni Serikali inayojali wanyonge, hatuwezi kumvumilia mtu ambaye ananyanyasa
wananchi; kama huna uwezo wa kulipa fidia usiombe leseni," alisisitiza
Nyongo.
Alimuagiza
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda husika na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Wilaya ya Manyoni kukutana na wananchi wenye malalamiko ili hatua stahiki
zichukuliwe na haki itendeke.
"Taratibu
za kumilikisha watu maeneo zifuatwe ikiwemo suala la ulipaji wa fidia,"
aliagiza Waziri Nyongo.
Aidha,
Waziri Nyongo alimuagiza Kamishna wa Madini kutenga maeneo zaidi kwa wananchi
wenye nia ya kuchimba Madini ya Jasi.
Naibu
Waziri Nyongo yupo Mkoani Singida kwa ziara ya siku Tatu ya kutembelea shughuli
za uchimbaji wa Madini mkoani humo na kuzungumza na wachimbaji ili kubaini
changamoto zinazowakabili kwa lengo la kutafutia ufumbuzi.
-Mwisho-
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.