KWA HISANI YA Parstoday Swahili
Wapiganaji 11 wa kundi moja la wanamgambo katika Jamhuri yya Kidemokrasia ya Congo wanaojiita 'Jeshi la Yesu' wamehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji.
Taarifa ya mahakama imesema kuwa, wanamgambo hao akiwemo kiongozi wao Fréderic Batumike ambaye ni Mbunge wa Kivu Kusini wamepatikana na hatia ya kuwabaka makumi ya wasichana wadogo akiwemo mtoto mdogo wa mwaka mmoja na nusu.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, kwa uchache wanamgambo hao 11 wa Jeshi la Yyesu waliwabaka wasichana wadogo 37 jirani na kijiji cha Kavumu katika Jimbo la Kivu Kusini baina ya mwaka 2013 na 216.
Fréderic Batumike alimuajiri mganga ambaye aliwapa ushauri wanamgambo hao kwamba, kama wangewabaka wasichana wadogo basi hilo lingewakinga na maadui zao.
Aidha kwa mujibu wa mahakama iliyotoa hukumu hiyo ni kwamba, hatia nyingine ya wanamgambo hao akiwemo Fréderic Batumike ni ya mauaji.
Mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu yameipongeza hukumu ya mahakama hiyo ambayo wameitaja kuwa ni ya kihistoria hasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo vitendo vya ubakaji vinavyofanywa na makundi ya wabeba silaha limekuwa ni jambo la kawaida na wahusika huwa hawaadhibiwi.
Raia wameomba mali za mbunge huyo zitaifishwe na kisha wapewe waathirika wa kitendo hicho cha ubakaji ili waweze kujimudu kimaisha.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.