Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza kwenye mkutano na Wananchi na Wachimbaji Wadogo kutoka Kata ya Silambo Wilayani Kaliua (hawapo pichani).
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa sita kushoto waliosimama mbele) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya ya Kaliua, Maafisa kutoka Ofisi ya Madini, Tabora na viongozi wa Mgodi wa Dhahabu wa Nsungwa Gold Mine uliopo katika Kata ya Silambo Wilaya ya Kaliua.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akielekea kwenye machimbo ya dhahabu yaliyopo katika Kata ya Silambo Wilayani Kaliua.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa tatu kutoka kulia) akitazama moja ya shimo la dhahabu lililoko katika Mgodi wa Nsungwa Gold Mine uliopo katika Kata ya Silambo Wilayani Kaliua.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (mbele) akielekea kwenye machimbo ya dhahabu yaliyopo katika Kata ya Silambo Wilayani Kaliua.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (mbele) akiongoza ujumbe wake kukagua shughuli za uchimbaji wa dhahabu kwenye mgodi wa dhahabu wa Nsungwa Gold Mine uliopo katika Kata ya Silambo Wilayani Kaliua.
WAKAGUZI WA MIGODI KUPUNGUZA AJALI
MIGODINI
Wakaguzi
wa Migodi Nchini wameagizwa kutembelea mara kwa mara kwenye migodi hususan ya
wachimbaji wadogo kwa ajili ya kukagua hali ya usalama na kuwasaidia Wachimbaji
kuepusha ajali wakati wa utekelezaji wa shughuli zao.
Agizo hilo
limetolewa Desemba 14, 2017 Mkoani Tabora na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus
Nyongo alipotembelea kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Nsungwa Gold Mine uliopo katika
Kata ya Silambo Wilaya ya Kaliua ili kujionea shughuli zinazofanywa mgodini
hapo na kuzungumza na wachimbaji.
Baadhi ya
Wachimbaji walimueleza Naibu Waziri Nyongo kuwa wamekuwa wakifanya shughuli zao
katika mazingira magumu bila kuwa na elimu ya namna bora ya uchimbaji wa
madini.
Nyongo
alisema ni jukumu la Maafisa Madini wakiwemo Wakaguzi wa Migodi (Mining
Inspectors) kuhakikisha wachimbaji hususan wadogo wanapatiwa elimu ya mara kwa
mara kuhusu afya, uchimbaji salama na uhifadhi wa mazingira ili kuepusha
magonjwa na ajali zinazosababishwa na uelewa finyu wa uchimbaji bora.
“Wachimbaji
wadogo wanapaswa kutembelewa na kuelimishwa mara kwa mara na hili ni jukumu
lenu, msisubiri hadi kutokee madhara ndio mfike kutoa elimu,” alisema.
Aidha,
Nyongo aliagiza wamiliki wa machimbo kuhakikisha wanawapatia vitendea kazi
wachimbaji kwenye maeneo yao ili kuwalinda na madhara yanayoweza kujitokeza
wakati wa utekelezaji wa shughuli zao.
Alisema
suala la kuwapatia vitendea kazi wachimbaji litasaidia kuepukana na ajali na
wakati huohuo kuchangia kuongezeka kwa mapato yatokanayo na shughuli hiyo ya
uchimbaji madini.
“Inabidi
muelewe, mnapowapatia vifaa hawa wachimbaji wenu mtaepukana na ajali kwahiyo
muda mwingi mtatumia kwenye kuzalisha na hivyo uzalishaji utaongezeka sambamba
na mapato yenu,” alifafanua Naibu Waziri Nyongo.
Vilevile
Nyongo alisisitiza umuhimu wa wachimbaji hao kujiunga katika vikundi ili kuwa
na urahisi wa kusaidiwa kuwa na uchimbaji wenye tija kwao na taifa kwa ujumla.
"Mkijiunga
kwenye vikundi itakua ni rahisi kuwafikia kwa pamoja na kuwapatia misaada
mbalimbali yenye tija kwenye shughuli zenu," alisema.
Aliongeza
kwamba dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Wachimbaji Wadogo wa Madini wanafanikiwa
kufikia kwenye uchimbaji wa Kati na baadaye kuwa Wachimbaji Wakubwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.