Katika kuepuka Misuguano ya kidini ambayo huenda ingeweza kuleta hali ya uvunjifu wa amani kwenye jamii ya watanzania Serikali kupitia Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza imelazimika kuandaa mafunzo kwa viongozi wa dini, yenye lengo la kuwakumbusha misingi inayotakikana katika uanzishwaji na uendeshaji taasisi hizo.
Mkutano wa viongozi wa Dini kupata mafunzo hayo ya jinsi ya kusajili taasisi zao kwa taratibu za Serikali umefanyika mkoani Mwanza ndani ya ukumbi mkubwa wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Kikao hiki kimeandaliwa na kamati ya Amani Mkoani Mwanza na kumkaribisha Mwana Sheria kutoka Wizara ya Mambo Ndani Ndugu Berias Nyansebwa, nao Viongizi wa Dini wakaelezwa juu ya dhana ya Uhuru wa kuabudu, Taratibu za usajili kabla ya kusajili na baada ya usajili.
Jeh ni manufaa gani viongozi wetu wa dini wanayoyaona kupitia mafunzo hayo.....
PICHA NA ZEPHANIA MANDIA WA GSENGO BLOG.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.