Rais Mohamed Abdullahi Mohamed wa Somalia jana Jumatano
alikataa pendekezo la Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia la
kujiunga na muungano wa nchi kadhaa za Kiarabu zilizoisuia Qatar na
kuiwekea vikwazo na badala yake Rais wa Somalia ametoa wito wa
kutatuliwa mgogoro huo kwa njia ya mazungumzo.
Ripoti ya tovuti ya Gulf Times imesema kuwa, mbali na kupinga mashinikizo hayo dhidi ya Qatar, Somalia pia imeziruhusu ndege za nchi hiyo kutumia ardhi na anga ya Somalia kwa ajili ya safari za kimataifa.
Kufuatia msimamo huo wa Somalia, serikali ya Imarati imezidisha harakati zake hasi katika maeneo yanayojitawala ya Somaliland na Puntland ambayo serikali ya Mogadishu inasisitiza kuwa ni milki na ardhi yake.
Mfalme Salman wa Saudi Arabia.
Saudia pamoja na nchi tatu za Kiarabu wapambe wake zilikata uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar kwa tuhuma kwamba nchi hiyo inaunga mkono ugaidi na haifuati sera za Baraza la Ushirikiano wa Ghuba ya Uajemi linaloongozwa na Riyadh katika mahusiano yake ya kigeni.

Qatar
inakadhibisha madai ya kuunga mkono ugaidi na inasisitiza kuwa, ni nchi
inayojitawala na kamwe haitafuata siasa za kiimla za Saudia.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.