Mbunge Godbless Lema.
Lema aliitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanahabari Mjini Arusha na kusema kuwa viongozi wa dini mbalimbali nchini wasifumbe macho yao na kujifanya hawayaoni mateso wanayopatiwa viongozi wa upinzani nchini.
"Viongozi wetu wa dini wasijifanye hili tunalofanyiwa upinzani hawayaoni. Kazi ya viongozi wa dini siyo kukemea bia na viroba bali wanatakiwa wapige kelele kwenye ukiukwaji wa misingi ya sheria inayoendelea hapa nchini dhidi ya upinzani", alisema Lema.
Pamoja na hayo, Mhe. Lema ameongeza kuwa viongozi wa dini endapo watasimama katika kukemea maovu yanayofanywa ndani ya nchi yakiwepo ya unyanyasaji watakuwa wamelikomboa taifa kwenye machafuko.
"Ipo siku kuna watu watashindwa kuvumiliwa haya tunayofanyiwa, hapo ndipo vita vya wenyewe kwa wenyewe vitakapokuja hapo siku za mbeleni" alimaliza
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.