MAOFISA wa serikali ya Sierra Leone wamesema
kuwa idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na maporomoko ya udongo na
mafuriko yaliyotokea Jumatatu iliyopita nchini humo imekaribia 500.
Ripoti iliyotolewa na serikiali ya Freetown imesema 156 kati ya waliofariki dunia ni watoto wadogo.
Shirika la Hilali Nyekundu la Sierra Leone limetangaza kuwa watu wasiopungua elfu tatu wamepoteza makazi yao kutokana na maafa hayo ya maporomoko ya udongo na mafuriko katika mji wa milimani wa Regent nje kidogo ya Freetown na kwamba watu wengine 500 hawajulikani waliko.
Rais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone ameomba misaada ya kimataifa kwa ajili ya wahanga wa maafa ya hayo.
Duru za hospitali za Sierra Leone zinasema kwamba, kuna upungufu mkubwa wa suhula za tiba na huduma za afya kwa majeruhiwa wa maafa hayo na hata mochari na nyumba za kuhifadhia maiti.

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.