WAZIRI wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye jana March
20, 2017 alifanya ziara makao makuu ya Clouds Media Group baada kuwepo
taarifa za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenda kwenye
kituo hicho akiwa na askari wenye silaha na kuwataka watangazaji wa
Kipindi cha SHILAWADU kurusha kipindi chake.
Waziri Nape aliunda Tume ya uchunguzi ya watu watano wakiongozwa na
Mkurugenzi wa Habari Maelezo na kutoa saa 24 kwa tume hiyo kuzungumza na
Makonda na watu wake kisha leo March 21 iwasilishwe.
Baasa ya kuona anapigiwa simu nyingi za kuhoji hatua iliyofikiwa hadi
sasa Waziri Nape ametoa majibu kupitia Account yake ya Twitter na kusema
’Kuna simu nyingi juu ya ripoti. Nawaomba tutulie Kamati wanamalizia
kazi yao, ikikamilika tutataarifiwa muda na mahali nitakapokabidhiwa!‘
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.