ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 21, 2017

WAZIRI MKUU WA SOMALIA: SAUDIA, MHUSIKA WA MAUAJI YA WAKIMBIZI WA SOMALIA.

Serikali ya Somalia imesema kuwa utawala wa Saudi Arabia ndio uliohusika na mauaji ya wakimbizi wa nchi hiyo katika maji ya Yemen.

Waziri Mkuu wa Somalia, Hassan Ali Khayre ametoa taarifa akilaani mauaji ya wakimbizi wa Kisomali yaliyofanywa na helikopta ya jeshi la Saudi Arabia karibu na pwani ya Yemen na kusema kuwa, wahanga hao wameuawa bila ya hatia yoyote na wengi wao walikuwa wanawake na watoto wadogo.

Waziri Mkuu wa Somalia ameitaka serikali ya Saudia pia kufanya uchunguzi kuhusu mauaji hayo.
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia, Abdisalam Omer amesema yaliyowakuta wakimbizi wasio na hatia yoyote wa Somalia ni maafa ya kushtua na kutisha na kusisitiza kuwa Saudi Arabia imehusika na jinai hiyo.
Miili ya Wasomalia waliouawa na Saudi Arabia.

Ripoti zinasema kuwa, wakimbizi hao wa Kisomalia waliokuwa katika boti wakielekea Yemen waliwasha tochi ili kuwaonesha askari wa Saudia kuwa si wanamgambo lakini helikopta ya jeshi la Saudia na meli moja ya kivita hazikujali alama hizo na badala yake ziliwamiminia risasi wakimbizi hao na kuwaua kikatili.

Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa limetangaza kuwa, wakimbizi wasiopungua 44 wa Somalia wameuawa katika shambulizi hilo na wengine 80 wamejeruhiwa.

Shirika la Kimataifa la Wahajiri (IOM) na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) yalilaani vikali mauaji hayo ya kinyama dhidi ya raia ambao hakuwa na silaha.  

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.