ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 3, 2016

NAIBU WAZIRI WA AFYA DK. KIGWANGALLA AFANYA ZIARA KATIKA HOSPITALI ZA WILAYA YA IRAMBA MKOANI SINGIDA.

dsc_0565
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisiliza maelekezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Iramba, Mkoani Singida wakati alipotembelea chumba cha upasuaji Hospitali hapo.

dsc_0571
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua vifaa vya Maabara 
dsc_0559
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Iramba namna wanavyokusanya mapato.
dsc_0584
Jengo la Utawala la Hospitali ya wilaya ya Iramba na juu  ni baadhi ya majengo ya Hospitali hiyo
dsc_0580
Picha chini ni Majengo ya Zahanati mpya ya Kisimba iliyopo Wilayani Iramba.
dsc_0592
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya Iramba Mkoani Singida na kukagua huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya pamoja na Zahanati ya Kisimba ndani ya Wilaya hiyo.

Katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla ameweza kubaini mapungufu mbalimbali ambayo ameagiza yapatiwe ufumbuzi ndani ya miezi mitatu.
dsc_0587
Akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba, ameweza kujionea huduma mbalimbali zitolewazo Hospitalini hapo hata hivyo ameagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanafunga mfumo wa ukusanyaji mapato wa malipo wa kisasa kwa njia ya kielektroniki.

“Mfumo wa malipo ya kielektroniki umeleta ukombozi mkubwa sana kwenye mahospitali nchini. Mapato yameongezeka. Udhibiti wa mapato umekuwa rahisi. 

Nawaagiza nanyi Hospitali ya Iramba kuhakikisha munafunga mfumo huu wa malipo wa kisasa hususani kwenye Maabara,Chumba cha upasuaji (Theatre), Dirisha la dawa, na sehemu zote zenye kuingiza mapato”. Ameeleza Dk.Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo hayo.

dsc_0593
Katika Zahanati ya Kisimba ambayo ipo umbali wa zaidi ya Kilometa 10, Dk.Kigwangalla ameweza kujionea huduma mbalimbali kwenye Zahanati hiyo ambayo ni mpya huku ikiwa msaada mkubwa kwa wananchi wa vijiji hivyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.