ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 4, 2016

WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUWA MGENI RASMI USIKU WA KUCHANGIA ELIMU JIMBO LA ILEMELA.

👊....... Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Angelina Mabula leo kazindua kampeni ya kuchangia Elimu, madawati na madarasa kwa wilaya yake ambapo itahitimishwa kwa awamu ya kwanza mnamo tarehe 9 July katika ukumbi wa Rock City Mall Mwanza, humo kutakuwa na Usiku wa kuchangia Elimu mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim.

Viongozi mbalimbali nao wameahidi kuhudhuria hafla hiyo akiwemo Waziri wa Fedha, Wabunge wote Kanda ya Ziwa bila kujali itikadi zao za vyama, viongozi mbalimbali wa dini, Taasisi za fedha, Makampuni na wafanyabiashara wameahidi kuhudhuria.
BOFYA PLAY KUSIKILIZA
Mhe. Angelina Mabula amesema, Lengo la Hafla hiyo ni kukusanya fedha na nyenzo za ujenzi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.5

📲Unaweza kuchangia zoezi hili kupitia mihamala ya fedha *

NAMBA YA AIRTEL - 0783474050
NAMBA YA VODA - 0763000608
NAMBA YA TIGO - 0719700400
JINA LITAKALOTOKEA :- ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL*


Huku mahojiano yakiendelea ndani ya kipindi cha KAZI NA NGOMA ilikuwa pia ni fursa ya kupata kumbukumbu. Kutoka kushoto ni G. Sengo, Mary Kimiti na Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Angelina Mabula
KAZI NA NGOMA na picha ya kumbukumbu na Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Angelina Mabula (kulia) wengine pichani ni Dvj Frank, G. Sengo na Mary Kimiti.
PAMOJA SANA 'Selfie'
CC:- @jembefm @OFFICEYAMBUNGEILEMELA @jembenijembe @dvjfrank @mary_kimiti @gsengo

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.