Duniani kote kwa sasa waislamu wanafanya ibada ya kutimiza moja kati ya nguzo zao tano za imani ya dini yao ya kiislamu, huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani na waislamu wote duniano hulazimika kufunga kama sehemu ya ibada yao, inawezekana uwaka hujui mtu wangu ila nakuletea TOP 10 ya mastaa wa soka ambao wanacheza mechi za Euro 2016 wakiwa wamefunga.
1- Emre Can
Anaichezea timu ya taifa ya Ujerumani
2- Xherdan Shaqiri
Huyu pia anaichezea timu ya taifa ya Switzerland ambayo tayari imetolewa
3- Granit Xhaka
Anaichezea timu ya taifa ya Switzerland ambayo imetolewa mapema katika michuano ya Euro 2016
4- Bacary Sagna
Bacary Sagna huyu anaichezea timu ya taifa ya Ufaransa
5- Arda Turan
Arda Turan anaichezea timu ya taifa ya Uturuki ambayo ilishatolewa katika michuano ya Euro 2016
6- Paul Pogba
Paul Pogba bado timu yake ya taifa ya Ufaransa ipo katika michuano ya Euro 2016
7- Stephan El Shaarawy
Stephan El Shaarawy anaichezea timu ya taifa ya Italia ambayo imetolewa katika hatua ya robo fainali na Ujerumani.
8- Mesut Ozil
Ozil anaichezea timu yake ya taifa ya Ujerumani na bado ipo katika michuano ya Euro 2016
9- Nuri Sahin
Timu yake ya taifa ya Uturuki ilishatolewa katika michuano ya Euro 2016
10- Sami Khedira
Anaichezea timu ya taifa ya Ujerumani ambayo imeingia katika hatua ya nusu fainali.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.