Video kwa hisani ya TBC 1
Emmanuel Amasi
Musoma Mara.
Ni moja kati ya matukio ya kusisimua ya mauaji yaliyitokea hapa nchini ambapo watu 17 wa familia tatu za ukoo mmoja wakiwemo watoto wadogo waliuawa kikatili kwa kukatwakatwa mapanga na kuchinjwa na watu wasiojulikana katika mtaa wa Bhugharanjabho Kata ya Buhare katika Manispaa ya Musoma, mkoani Mara.
Waliofanya mauaji hayo pia walikatakata ng’ombe na mbuzi katika sehemu mbalimbali na kuacha mizoga hiyo imetapakaa ovyo ovyo katika miji hiyo.
Tukio hilo la kutisha na la kwanza kutokea mkoani Mara, lilitokea mnamo mwaka 2010 na ilikuwa majira ya saa sita na nane usiku wa kuamkia february 16, kwa kuhusisha familia tatu za ukoo mmoja huku watu wengine saba wakijeruhiwa vibaya na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mara.
Familia ambayo ilikumbwa na tukio hilo la kusikitisha ni za Kawawa Kinguye ambapo mke na watoto wake watano akiwemo yeye mwenyewe waliuawa wakati katika familia ya mdogo wake, Moris Mgaya watu sita pia waliuawa na kwa binamu yake, Mgaya Nyarukende watu watano waliuawa.
SITOSAHAU.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.