Mmoja wa polisi waliojeruhiwa, waliletwa Nairobi kwa matibabu |
Maafisa hao walivamiwa katika eneo la Baragoi, kaunti ya
Samburu, Kaskazini mwa nchi.
Msemaji wa polisi aliambia BBC kuwa polisi 29 waliuawa pamoja na
washambuliji watatu , lakini viongozi wa kijiji wanahofia kuwa huenda maiti
zaidi wakapatikana. Hii leo miili zaidi ilipatikana na kufikisha idadi ya
polisi waliouawa kuwa 40.
Wenyeji wa eneo hilo wana historia ya kupigana kwa sababu ya
uhaba wa malisho ya mifugo wao. Wiki mbili zilizopita, watu 12 waliuawa katika shambulizi kama
hilo kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya.
Haya yanasemekana kuwa mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kutokea
dhidi ya polisi tangu Kenya kujipatia uhuru wake. Maiti 11 walipatikana siku ya Jumamosi na wengine 19 kupatikana
Jumapili.
Inspekta wawili wakuu wa polisi wangali hawajulikani waliko. Uvamizi huu ni pigo kubwa kwa idara ya ulinzi nchini. Baadhi ya
polisi waliviziwa na kuuawa na wezi wa mifugo, katika eneo la Lomerok. Manusura
tisa wangali wanapokea matibabu hospitalini.
Mauaji haya yanafikisha idadi ya watu waliouawa katika eneo hilo
katika wiki mbili zilizopita hadi 43.
Aidha mashambulizi haya yanatokea huku shughuli ya kuajiri
inspekta mkuu wa polisi ikiendelea sambamba na polisi kususia kazi kwa sababu
ya mzozo wa mishahara.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.