ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 25, 2011

ANG'ATWA SIKIO NA MHUDUMU WA BAR KISA TOOTHPICKS!!

Matokeo ya hiki ukionacho ni kutoka katika Tukio lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika bar moja maarufu kwa kuuza 'mdudu' jijini mwanza maeneo ya Kilimahewa iitwayo 'AR Pub', ambapo kaka mwenye sikio lake zimaaa!.. aling'atwa akiwa nje ya bar katika harakati za kutafuta usafiri wa pikipiki kuelekea anakokujua ikiwa ni mara baada ya kupata huduma ya chakula akipendacho ndani ya bar hiyo na kisha kulipa vizuri tu. Sheshe lilikuja mara baada ya wawili hao kuzama katika majibizano yaliyo jaa kejeli yaliyotokana na mteja huyo mwenye sikiong'atwa hapo juu kunyimwa kwa maksudi njiti hizo za kusafishia meno aka 'tuthi piki'.

Mteja :: Utaniambia nini wewe si k..a tu!

Muhudumu :: Wewe Ms..e unasemaje?

Haikuchukuwa raundi kwa mhudumu kuimiliki shingo ya mteja kwa kumpiga roba (kabali), nyonga-nyonga, niga-niga....!!...!!

Mteja :: 'aaagh NIACHIE'

Mhudumu :: 'SIKUACHII'. Hamadi sikio hili hapa mhudumu akapata 'aNaZa aIdIa' akaling'ata akilisigina kwa meno hadi likakatika 'nkwachu' kisha akalitema ppTuU!!

Tupe maoni yako

2 comments:

  1. Duh! ni hatari kwenda kwenye hiyo bar kama mambo yanyewe ndo hivyo. Pole kwa kungátwa na sikio....

    ReplyDelete
  2. Ukitaka kula nenda mgahawani, Bar kuna mengiii. Pole sana.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.