HABARI NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO, PWANI
SAUTI NA ALBERT G.SENGO Wananchi zaidi ya 120 wa kitongoji cha Kwakibosha Kata ya Mapinga Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani wameiomba Serikali kuingilia kati sakata la kukithiri kwa wimbi la matapeli wa ardhi ambao wamekuwa wakiwanyanyasa na kuwaonea kwa kipindi cha muda mrefu ikiwemo kuwavunjia nyumba zao za makazi na kupelekea kukosa maeneo ya kuishi. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa mkutano maalmu wa hadhara wamesema kwamba kwa sasa wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu kutokana na nyumba zao 12 kubomelewa na mmoja wa wanannchi anayejulikana kwa jina la Peter Junior na kuomba mamlaka zinazohusika achukuliwe hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine. Kwa upande wake Mwenyekiti wa kitongoji cha Kibosha Shaban Rashid akizungumzia kuhusiana na hatma ya wananchi juu ya mtu huyo anayedaiwa kuwasumbua kwa muda mrefu amebainisha kusikitishwa kwake na vitendo vinavyofanywa na mtuhumiwa huyo ambaye amekuwa akiwanyanysa wananchi kwa kuwavunjia nyumba zao.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.