ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 27, 2019

NAIBU MEYA JOSEPH RYATA: KUIMARISHA MIUNDOMBINU KUTASAIDIA KUKUZA UCHUMI WA MANISPAA YA IRINGA.

Naibu meya wa manispaa ya Iringa kupitia chama cha mapinduzi Joseph Ryata akizungumza na wananchi wa kata ya Ruaha na Kitwiru juu ya maendeleo ya manispaa ya Iringa na kuwaambia mikakati yao.
Baadhi ya wananchi wa Manispaa ya wakiwasikiliza madiwani wa chama cha mapinduzi wakielezea sera zao na mikakati juu ya maendeleo ya manispaa ya Iringa.


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
 
Naibu meya wa manispaa ya Iringa kupitia chama cha mapinduzi Joseph Ryata amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya uchumi ili kukuza ukchumi kwa wananchi na kuleta maendeleo kwa taifa.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Ruaha,Ryata alisema kuwa watahakikisha barabara  zote za manispaa ya Iringa zinapitika kirahisi ili kuhakikisha kuwa zinapitika na zinakuwa rafiki kwa wafanyabiashara kufanya biashara zao.

“Wananchi tusipokuwa na miundombinu bora ya barabra hatuwezi kufanya biashara na kupata maendeleo yanayaotakiwa hivyo ni lazima tuwasimamie viongozi wetu wa serikali kuhakikisha barabara zote zinapitika bila kuwa na vikwazo kwa wafanyabiasha na wananchi kwa ujumla” alisema Ryata

Ryata aliongeza kuwa madiwani wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa wamejipanga kuhakikisha kuwa wanasimamia vilivyo ujenzi wa gorofa katika maeneo ya standi ilipokuwa tembo bara na kuboresha kwa kuujenga upya ukumbi wa Community center ulipo katika kata ya Kitanzini Miomboni na kujenga hoteli ya kitalii katika kata ya Gangilonga.

“Tukiboresha miundombinu hiyo yote na kujenga majengo ya kibiashara yatatusaidia kukuza uchumi wa wananchi wa manispaa ya Iringa na nje ya manispaa ya Iringa hivyo mipango hii inasimamiwa vilivyo na madiwani wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa” alisema Ryata

Ryata aliwataka wananchi wa manispaa ya Iringa kuhakikisha wanaendelea kuwachagua viongozi wa chama cha mapinduzi ili waweze kusaidia kuleta maendeleo kwa haraka na ubora unaotakiwa tofauti na viongozi wengi wa upinzani  hawana hoja za kiuchumi.

Naye diwani wa kata ya Ruaha Tandesi Sanga alisema kuwa wamefanikiwa kuboresha miundombimu ya sekata ya afya,elimu pamoja na miundombinu ya uchumi kwa lengo la kuhakikisha wananchi wa kata hiyo wanafanya kazi za maendeleo bila ya kuwa na usumbufu wowote ule.

“Nyie mashaidi toka nimekuwa diwani wa ccm tumefanikiwa kuboresha sekta ya elmu kwa kuboresha miundombinu ya majengo ya shule zetu za sekondari na msingi na zahanati zetu tumeziboesha mno hivyo lazima tufanye kazi kama Rais wetu anavyotutaka” alisema Sanga

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.