Mkurugenzi wa wilaya ya Ileje Haji Mnasi akishiriki ujenzi na upanuzi wa hospitali ya wilaya ya ileje akiwa sambamba na mafundi wengine
Mkurugenzi wa wilaya ya Ileje Haji Mnasi akishiriki ujenzi na upanuzi wa hospitali ya wilaya ya ileje akiwa sambamba na mafundi wengine
NA FREDY MGUNDA,ILEJE
MKURUGENZI wa wilaya ya Ileje Haji Mnasi ameshiriki
ujenzi na upanuzi wa hospitali ya wilaya ya ileje baada ya kupokea kisai cha
shilingi bilioni 1.5 kutoka serikalini ili kuhakikisha hospitali hiyo inajengwa
kwenye ubora unaotakiwa na wananchi wanapata huduma bora za kiafya.
Akizungumza wakati wa ujenzi huo Mnasi alisema
kuwa lengo la kushiriki ujenzi huo ni kuhakikisha anaweka hamasa kwa mafundi na
wananchi kusimamia vilivyo kuhakikisha hospitali hiyo inajengwa kwa kiwango
kinachotakiwa na serikali kuu.
“Mimi kama kiongozi lazima niwe mfano wa kuigwa
kwa kufanya kazi kwa vitendo hivyo kuja kwangu kushiriki ujenzi huu ni
kuonyesha jinsi gani tunatakiwa kufanya kazi tuliyoagizwa na Rais wetu” alisema
Mnasi
Mnasi alisema kuwa atahakikisha bega kwa bega katika
usimamizi na ushiriki wa karibu kuhakikisha ujenzi unakamilika na thamani
ya fedha(value for money) kwa wakati ili kutimiza malengo ya serikali
yanayokusudiwa.
“Nikija mara kwa mara kuangalia ujenzi huu
nitahakikisha ujenzi ulio bora wa kuzingatia ujenzi unaofaata hatua zote za
msingi na kupata majengo yaliyobora ya hospitali hii ya wilaya” alisema Mnasi
Lakini pia mkurugenzi Haji Mnasi aliishukuru na kuipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Pombe Magufuli kwa kuwajali wananchi kwa kutoa kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.