MIFUKO ya plastiki al-maarufu kama 'RAMBO' (hapa Tanzania) inalaumiwa pakubwa kwa uchafuzi wa mazingira duniani, na harakati za kukomesha matumizi yake yanalenga kulinda mazingira.
Kwa kuliheshimu hilo Juni 1, 2019 itakuwa ni kosa la jinai kutengeneza, kuagiza, kusambaza na kutumia mifuko ya plastiki nchini Tanzania, na wote watakao kaidi marufuku hiyo watakutana na mkono wa sheria.
Marufuku hiyo inahusisha maeneo yote ya Tanzania Bara, upande wa pili wa muungano Visiwa vya Zanzibar vinatekeleza marufuku hiyo kwa miaka kadhaa sasa.
Tanzania Bara pia imekuwa katika harakati za kupiga marufuku mifuko ya plastiki kwa zaidi ya mwongo mmoja huku harakati hizo zikikwama mara kadhaa.
Safari hii serikali imeonekana kujidhatiti kutekeleza marufuku hiyo kama wafanyavyo nchi jirani za Rwanda na Kenya ambapo Halamashauri za mikoa na wilaya mbalimbali nchini nazo zinafanya jitihada zake kulifanikisha zoezi hilo.
Jeh Jijini Mwanza kunani?
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.