ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 7, 2017

UPINZANI KONGO DR WAPINGA TAREHE YA UCHAGUZI ILIYOTANGAZWA NA CENI.

Upinzani Kongo DR wapinga tarehe ya uchaguzi iliyotangazwa na CENIVyama vya upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo vimepinga tarehe ya uchaguzi iliyopendekezwa na Tume ya Uchaguzi CENI hivi karibuni.

Augustin Kabuya, msemaji wa chama kikuu cha upinzani nchini humo UPDS amesema, "hatukubaliana na ratiba ya uchaguzi iliyotolewa na CENI, tunachotaka kuona kikifanyika ni Rais Joseph Kabila aachie ngazi kabla ya Disemba 31 mwaka huu." Mwisho wa kunukuu.

Kinara wa upinzani nchini humo Moise Katumbi ambaye kwa sasa yuko nje ya nchi ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa "Hatukubaliana na tarehe hiyo ya serikali ambayo ipo mamlakani kinyume cha sheria. Wanataka tu kuona hakuna uthabiti Kongo huku wakiwahangaisha wananchi. Kabila lazima aondoke." Mwisho wa kunukuu.

Rais Joseph Kabila wa DRC 
 
CENI siku ya Jumapili ilisema kuwa uchaguzi wa rais wa kumtafuta mrithi wa Rais Joseph Kabila utafanyika Disemba 23, mwaka ujao wa 2018.
 
Mkuu wa tume hiyo, Corneille Nangaa amewaambia waandishi habari mjini Kinshasa kuwa watu 43 milioni wamesajiliwa kama wapiga kura nchini humo hadi sasa, na kwamba matokeo ya uchaguzi huo yatatangazwa Januari 9 , 2019 na rais kuapishwa Januari 13.

Uchaguzi huo ulikuwa umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2016 na umeakhirishwa mara kadhaa kufikia sasa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.