Wanafunzi wa darasa la tano wakimsikiliza kwa makini mwalimu wa taaluma.
Wanafunzi wa darasa la sita na la saba katika wa shule ya Genius Kings wakiwa katika chumba cha maabara wakijifunza somo la sayansi kwa vitendo.
Wanafunzi wa darasa la sita na la saba katika wa shule ya Genius Kings wakiwa katika chumba cha maabara wakijifunza somo la sayansi kwa vitendo wakitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Shule hiyo Bw. Machage Kisyeri.
Mkurugenzi wa Shule hiyo Bw. Machage Kisyeri akiwa ofisini kwake.
Shule
ya awali na ya msingi ya Genius Kings iliyopo Tabata-Segerea jijini Dar
es Salaam imejizatiti kuhakikisha inakuwa shule bora na ya mfano
kitaaluma ikiwa ni mwendelezo wa mafanikio ambayo imeyapata katika
kipindi cha miaka 10 tangia kuanzishwa kwake.
Akiongea
jijini Dar es Salaam kuhusiana na maadhimisho ya miaka 10 tangu
kuanzishwa kwake ambayo yameanza kusherehekewa mapema wiki na kutarajia
kumalizika mapema mwezi Desemba mwaka huu,Mkuu wa shule hiyo,Bw.Aloyce
Siame,alisema licha ya kwamba mwanzo huwa ni mgumu kwa mradi wowote ule,
shule imeweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika
sekta ya elimu na kuweza kuchomoza kuwa miongoni mwa shule zinazofanya
vizuri mkoani Dar es Salaam na kwa ngazi ya kitaifa.
Bw.Siame
alisema kuwa katika kipindi cha miaka 10 shule imeweza kushikilia
rekodi ya kufanya vizuri kwa kufaulisha wanafunzi wa darasa la saba na
la nne kwa kiwango cha juu na kuingia katika shule tano bora wilayani
Ilala na shule bora 20 mkoani Dar es Salaam mfululizo hali ambayo
imewajengea hari ya kuzidi kufanya vizuri kwa mwaka huu na miaka ijayo.
“Moja
ya mtazamo wa shule hii ni kuifanya kuwa shule bora ya mfano inayotoa
elimu bora nchini kuanzia shule ya awali na shule ya msingi.Tumejipanga
kuhakikisha lengo hili linatimia na tunatoa shukrani kwa serikali,wazazi
na wadau wote ambao wameonyesha kutuunga mkono katika kipindi hiki cha
awamu ya kwanza ya mwanzo ya miaka 10 na kuwezesha mafanikio haya
kupatikana”.Alisema.
Aliongeza
kuwa mbali na kufundisha masomo ya darasani kwa nadharia na vitendo na
ujuzi wa kutumia kompyuta kupata maarifa ya kielimu shule inatoa mafunzo
ya kuwajengea wanafunzi uwezo wa kuwa wabunifu,Sanaa,michezo
mbalimbali,kuwajengea uwezo wa kujiamini kuongea mbele ya hadhara na
kufanya mijadala ya kuchambua masuala yanayohusiana na elimu na nyanja
nyinginezo hususani masuala yanayoendelea hapa nchini na nje ya nchi
bila kusahau kuibua na kukuza vipaji vya wanafunzi.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa shule hiyo,Bw.Machage Kisyeri,alisema
anajivunia kwa mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka 10 na
kuahidi kuwa uongozi umejipanga kuhakikisha kitaalamu shule inazidi
kupanda zaidi na kuimarisha mafunzo ya shule ya awali kwa ajili ya
kuwaandaa wanafunzi wadogo kupata elimu bora zaidi kwa kutumia nyenzo
mbalimbali za kisasa,kuimarisha miundombinu na kuongeza walimu wenye
ujuzi mkubwa wa kufundisha madarasa ya chini ya watoto wadogo kwa kuwa
msingi mzuri kielimu ndio unawezesha watoto kuendelea kufanya vizuri
katika masomo yao.
Kuhusiana
na changamoto wanazokabiliana nazo alisema kuwa zipo changamoto za
kawaida kinachotakiwa ni ushirikiano baina ya wazazi,walimu,na wadau
wanaosimamia elimu ili kuhakikisha mafanikio yanapatikana na elimu ya
Tanzania inazidi kupanda “Walimu wakiwezeshwa vizuri na kupewa
ushirikiano wa kutosha naamini shule nyingi za Tanzania zitatoa elimu
bora kwa kuwa tunao walimu wengi wazuri ambao wakitumiwa ipasavyo
tutasonga mbele”.Alisema.
Akiongea
kwa niaba ya wanafunzi wenzake,Mwanafunzi John Magongo anayesoma darasa
la saba shuleni hapa alisema kuwa wanawezeshwa kupatiwa elimu ya
kuwajengea uwezo wa kufanya vizuri kitaaluma ,nidhamu, kujiamini na
kujituma kiasi kwamba popote watakapokwenda wanaamini watazidi kung’ara
kutokana na elimu inayotolewa shuleni hapo.
Shule
ya Genius Kings ilianzishwa mnamo mwaka 2008 na vijana wa kitanzania
wenye taaluma mbalimbali ambapo waliweza kupata walimu wazuri ambao kwa
kipindi chote hiki wamewezesha kupatikana mafanikio ya shule kuwanoa
wanafunzi vizuri kitaaluma na kuwa miongoni mwa shule bora mkoani Dar es
Salaam ,pia uwekezaji wa shule hii umewezesha kupunguza tatizo la ajira
kwa kuwa mbali na kuajiri walimu imeajiri wafanyakazi katika vitengo
vyake mbalimbali vya uendeshaji.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.