Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (aliyesimama)
akifungua
Warsha ya Siku Mbili ya Wadau wa Vyama vya Ushirika inayoendelea katika
Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. Wengine pichani
ni Mkurugenzi wa Benki Kuu Tawi la Mtwara, Bw. Lucas Mwimo (kushoto) na
Kaimu Katibu Tawala Msaidizi – Uchumi na
Uzalishaji, Bw. Amani Rusake (kulia).
Mkurugenzi wa Biashara wa Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha akiwasilisha mada
kuhusu mchango wa TADB katika mapinduzi ya kilimo nchini.
Mwakilishi wa Mrajis wa Vyama vya Ushirika Nchini, Bw. Nerei Kyara akizungumza na Wadau wa Vyama vya Ushirika wakati wa Warsha ya Siku Mbili ya Wadau inayoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. Wengine pichani ni Kaimu Katibu Tawala Msaidizi – Uchumi na Uzalishaji, Bw. Amani Rusake (kushoto) na Mkuu wa Kilimo na Fedha Vijijini wa Mfuko wa Kukuza Sekta ya Fedha, Bw. Mwombeki Baregu.

Wadau wa Vyama vya Ushirika wakifuatilia mijadala mbalimbali wakati wa Warsha
ya Siku Mbili ya Wadau inayoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Wadau wa Vyama vya Ushirika wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa Warsha ya Siku Mbili ya Wadau hao inayoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
Na Mwandishi wetu, Mtwara
Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imewaasa wakulima wa korosho
nchini
kuongeza uzalishaji wa korosho ili kuchangamkia fursa za masoko ya zao
hilo linalohitajika zaidi katika masoko ya Marekani, Vietnam na India.
Wito
huo umetolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis
Assenga
wakati akifungua Warsha ya Siku Mbili ya Wadau wa Vyama vya Ushirika
inayoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Mtwara.
Bw.
Assenga alisema kuwa mahitaji ya korosho ni makubwa sana katika soko la
dunia
hivyo wakulima wa zao hilo hawana budi kujizatiti ili kuhakikisha
wanazalisha kiasi kikubwa cha korosho ili kufikia au kuzidi malengo ya
mavuno kwa msimu ujao ambayo yanakadiriwa kufikia kati ya tani laki tatu
(3) hadi laki nne (4) ukilinganisha na takribani
tani laki mbili na nusu kwa msimu uliopita.
Bw. Assenga alisema kuwa korosho ni zao la kimkakati ambalo likiwekezwa kwa usahihi
linaweza kunyanyua uchumi na kipato kwa wakulima wa mikoa ya kusini na pwani ambao niyo ni wazalishaji wakuu wa zao hilo.
“Nawaasa mujitahidi kulima kisasa ili kuweza kufikia au kuvuka malengo ya mavuno
ya msimu huu hali itakayowaongezea kipato hivyo kufikia malengo ya serikali ya kuwanyanyua wakulima nchini,” alisema.
Kaimu Mkurugenzi huyo wa TADB aliongeza kuwa Benki yake imejipanga kusaidia mfumo
wa Stakabadhi ya maghala ili kuhakikisha kuwa malengo ya mavuno ya korosho kwa msimu huu yanafikiwa.
“TADB
iko tayari kuratibu mfumo wa malipo ya fedha zitokanazo na mauzo ya
korosho
kwa njia ya TEHAMA, pia kwa kushiriakiana na soko la mazao (TMX),
kusimamia ununuzi wa mazao kwa njia ya mtandao (electronic auction),”
aliongeza
Aliongeza kuwa Benki ipo tayari kusimamia uuzaji wa mazao kwa mifumo ya salama
ya kimataifa ya malipo kama vile dhamana ya malipo.
Naye Mkurugenzi wa Biashara wa Mikopo wa
TADB, Bw. Augustino Chacha alisema kuwa
Benki ya Kilimo ipo tayari kutoa mikopo kwa ajili ya uendelezaji wa
miundombinu ya umwagiliaji na maghala na uzalishaji wa mbegu bora za
mazao ya korosho na mihogo.
Aliongeza kuwa TADB pia ipo tayari kuviwezesha
viwanda vya kubangua mazao ya korosho, na kusindika ufuta, mihogo
pamoja na uanzishaji wa mashamba mapya na ya kisasa ya korosho na
ufuta.
“Tupo
tayari kutoa mikopo kwa ajili ya kuwanyanyua wakulima kama ilivyolengwa
na Serikali kupitia mikopo ya pembejeo kuongeza tija kwenye uzalishaji,
miundo mbinu ya umwagiliaji na ununuzi wa zana za kilimo (kama
matrekta, pump),” alisema.
Bw.
Chacha aliongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa uhifadhi wa mazao ya
kilimo,
Benki ya Kilimo ipo tayari kutoa mikopo kwa ajili ya kujenga maghala
mapya au kuboresha yaliyopo pamoja na kununua mizani ya kisasa na
ununuzi wa magari ya usafirishaji mazao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.