Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya
Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (kushoto) akizungumza na
aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mzee Peniel Lyimo
(kulia) wakati wa Kikao cha Wadau wa Kilimo
Kujadili Mikakati Ya Kuboresha Uwezeshaji Kwenye Kilimo Na Viwanda
kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNICC) Dar
es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Biashara ya TADB, Bibi Rehema Twalib (kulia) akizungumza wakati wa
Kikao cha
Wadau wa Kilimo Kujadili Mikakati Ya Kuboresha
Uwezeshaji Kwenye Kilimo Na Viwanda kinachofanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam.
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mzee Peniel Lyimo (kulia) akiongoza Kikao hicho.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) akisisitiza nafasi ya
Benki yake katika kuleta matokeo makubwa kwenye mapinduzi ya kilimo na viwanda hasa vya uchakakataji na usindikaji wa mazao
ya kilimo.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi,
Bibi Rosebud Kurwijila (kushoto) wakifuatilia kwa makini Kikao hicho.
Washiriki wa Kikao
hicho wakifuatilia mawasilisho mbali mbali wakati wa Kikao cha wadau wa
kilimo waliokutana kujadili mikakati ya kuboresha uwezeshaji kwenye
kilimo na viwanda. Kikao hicho kiliandaliwa
na Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB).
Wadau wa kilimo waliokutana kujadili mikakati ya kuboresha uwezeshaji kwenye kilimo na viwanda wakiwa katika picha ya pamoja.
Na Mwandishi wetu,
Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) imekutana na wadau wa kilimo ili kujadili
mikakati ya kuboresha uwezeshaji kwenye kilimo na viwanda katika
kuhakikisha Benki hiyo inasaidia sekta ya Kilimo iweze kusukuma dhamira ya Serikali ya kujenga Uchumi wa Viwanda.
Akizungumza
katika kikao hicho Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis
Assenga
amesema kuwa Benki imejipanga kuleta matokeo makubwa kwenye mapinduzi
ya kilimo na viwanda hasa vya uchakakataji na usindikaji wa mazao ya
kilimo.
Bw.
Assenga amesema kuwa mipango hii itasaidia upatikanaji wa mali ghafi
kwa viwanda
vya ndani hivyo kusukuma ndoto ya Serikali kufikia lengo lake la
Kujenga Uchumi wa Viwanda na kuhuisha uwekezaji kwenye Viwanda vidogo
vidogo na vya kati vya usindikaji na uchakataji wa mazao ya Kilimo na
mifugo.
“Benki
imejikita kwenye kusaidia Sekta ya Kilimo iweze kusukuma dhamira ya
Serikali
ya Uchumi wa Viwanda uweze kutoa matunda yaliyokusudiwa ili kuchagiza
na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha
kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,”
alisema.
Bw.
Assenga amesema katika kuhakikisha azma hiyo inatimia TADB imejipanga
kutoa elimu
ili kuwajengea uwezowakulima na taasisi mbali mbali za fedha pamoja na
vyama vya ushirika kuweza kukopa toka TADB pamoja na kushirikiana na
wadau mbali mbali kusaidia uwekezaji mkubwa kwenye Sekta ya Kilimo ili
iweze kuinua pato la Taifa na kumkomboa Mwananchi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo ameongeza kuwa TADB imeanza kujiimarisha
na kuchochea mabenki na taasisisi za fedha
kuongeza utoaji wa mikopo na fedha zingine kwenye Sekta ya Kilimo ili
kuongoza utoaji mikopo ya uongezaji wa thamani katika shughuli za
kilimo.
TADB ni taasisi ya
serikali ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu mkubwa wa
upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini
ambao ulikuwa unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo
mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa
biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo; mikopo ya muda
mfupi; masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia hali halisi ya sekta ya
kilimo
na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.