ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 14, 2017

NJOMBE WAJITOKEZA KUOKOA MAISHA YA MAMA NA MTOTO KWA KUCHANGIA DAMU.


AMIRI KILAGALILA
NJOMBE.
Wakati Akina Mama Wajawazito Wakionekana ni Kundi Linalokuwa na Uhitaji Mkubwa wa Damu Hasa Pindi Wanapojifungua hali inayopelekea baadhi yao kupoteza uhai au pengine kuhatarisha afya ya mama na mtoto, Jamii Mkoani Njombe Imetakiwa Kuwaonea Huruma Kwa Kujitokeza kwa wingi katika Kuchangia Damu.

Kila Juni 14  Ya Mwaka Tanzania Huungana na Mataifa Mengine Duniani Kuadhimisha Siku ya Uchangiaji Damu Ambapo Mkoani Njombe Kiwango Kikitajwa Kuwa Chini Cha Uchangiaji wa Damu na Kusababisha Madhara Kwa Wagonjwa Wakiwemo Akina Mama Wajawazito.

Katika Kuadhimisha Siku Hii Kituo Hiki Kimezulu Katika Hospitali ya Mkoa wa Njombe ya Kibena na Kufanya Mazungumzo na Baadhi ya Wananchi Waliojitokeza Kuunga Mkono Jitihada za Serikali za Kuwaokoa Wagonjwa Wanaopungukiwa Damu Kwa Kuchangia Damu Ambao Wanasema ni Vyema Jamii Ikawa na Moyo wa Huruma Kwa Kuwachangia Damu Wagonjwa.
Dokta Winfred Kyambile ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Njombe Ambaye Anasema Kiwango Cha Uchangiaji Damu Kimekuwa Chini Sana Kutokana na Uhamasishaji Duni Kwani Kwa Mwaka Uliopita ni Asilimia 16 Pekee ya Damu Iliyopatikana.

Kwa Upande Wake Mratibu wa Damu Salama Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Grace Matandala Amesema Jamii Imekuwa Ikiogopa Kujitokeza Kuchangia Damu Wakidhani Huenda Watapungukiwa Damu Mwilini Jambo Ambalo Halina Ukweli Wowote Kwa Kuwa Wanaotolewa Damu Ni Lazima Wawe na Sifa.

Hata Hivyo Kumekuwapo na Malalamiko ya Kuwa Damu Imekuwa Ikiuzwa Au Lazima Mgonjwa Awe na Ndugu Yake Anayeweza Kutolewa Damu Ndipo Apatiwe Damu Jambo Ambalo Limekanushwa na Uongozi wa Hospitali ya Kibena na Kwamba Damu Hutolewa Bure Pasina Malipo Yoyote Kwa Mgonjwa.
Mary Salum Mgaya ni Mmoja Kati ya Wenye Wagonjwa Katika Hospitali Hiyo Ambaye Naye Anakiri Kuwa Mgonjwa Wake Amepatiwa Huduma ya Damu Pasina Malipo Yoyote Hadi Sasa.

Lakini Wengine Wamesema Kauli za Kuwa Damu Inatolewa Bure Hazina Ukweli Wowote.




Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.