WATU wenye silaha wasiojulikana wametekeleza shambulizi katika soko nchini Sudan na kuua watu saba na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Habari nchini humo zinaarifu kuwa,
tukio hilo lilitokea Jumapili ya jana huko katika jimbo la Kordofan
magharibi ambapo watu wenye silaha wasiojulikana wakitumia magari ya
kiraia walishuka kutoka katika magari hayo na kuanza kuwafyatulia risasi
watu waliokuwa sokoni. Hadi sasa hakuna kundi lililotangaza kuhusika na
hujuma hiyo.
Rais Omar al-Bashir wa Sudan
Inafaa kuashiria kuwa, waasi wa majimbo ya Kordofan kusini na Blue
Nile wanapambana na jeshi la serikali ya Khartoum tangu mwaka 2011.
Mapigano huko Darfur, yalianza mwaka 2003 baada ya makabila ya eneo hilo
kuituhumu serikali ya Rais Omar al-Bashir wa Sudan kwa kufanya ubaguzi
dhidi yao. Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa,
katika mapigano yaliyojiri maeneo ya machafuko nchini humo, karibu watu
laki tatu waliuawa Darfur na zaidi ya wengine milioni mbili na laki tano
kuwa wakimbizi.
Madhara ya siulaha za kemikali zinazotajwa kutumiwa na jeshi la serikali dhidi ya raia
Kwa kawaida raia wa kawaida ndio huwa wahanga wa mashambulizi ya
waasi na askari wa serikali. Mwanzoni mwa mwezi Machi uliomalizika
shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lilitoa
wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu mashambulizi ya silaha za kemikali
yaliyofanywa na serikali ya Sudan dhidi ya raia wa kawaida katika eneo
la Darful, magharibi mwa nchi hiyo.
SANGU: BODI YA WADHAMINI WCF KUTEKELEZA DIRA 2050
-
Na. OWM-KAM – Dodoma
Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) imetakiwa kuweka
mikakati ya kuanza utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maende...

ENDORO WATER FALLS, MAAJABU MENGINE NGORONGORO
-
Mbaraka Mwinshehe aliwahi kuimba akiisifia Morogoro na jinsi maji
yanavyotiririka kutoka milimani.
Mwinshehe angekuwa hai pengine angefika maporomoko ...
0 comments:
Post a Comment