Wateja wa Airtel laki 4 wajisajili kupata huduma za afya bure
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na programu ya mHealth
Tanzania PPP (mHealth Tanzania Partnership) inayoratibiwa na Cardno
Tanzania chini ya ), ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia,
wazee na watoto kupitia mradi wa Wazazi Nipendeni wawawezesha wamama
wajawazito na wenye watoto wadogo takribani laki 4 kujiunga na kupata
taarifa mbalimbali za afya kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu bila malipo
yoyote pindi wanapojiunga na kupata jumbe hizi kupitia simu zao za
mkononi
Mradi
huo wa Wazazi Nipendeni ulioko chini ya Wizara ya Afya, maendeleo ya
jamii, jinsia, wazee na watoto umeanzishwa kwa lengo la kutoa elimu ya
afya na kuokoa vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano
ambavyo vilikuwa vinakuwa kwa kasi kwa sababu mbalimbali ikiwemo
kutokuwa na elimu ya kutosha juu wa maswala ya kiafya.
Akitoa
tathimini juu ya mradi huo mpaka sasa Bwn Mtasingwa Saulo kwa niaba ya
mHealth Tanzania Partnership alisema” mHealth Tanzania Partnership
imeshirikiana na Airtel toka mwaka 2012 katika kuhakikisha taarifa
mbalimbali za kiafya zinawafikia watanzania bila gharama yoyote. Mpaka
sasa mradi huu umekuwa na mchango mkubwa sana zaidi ya watumiaji laki 4
wameshajisaji na takribani meseji zaidi ya million 27 zenye taarifa
mbalimbali za afya zimetumwa bila gharama yoyote. Tunawashukuru sana
Airtel kwa kushirikiana nasi katika kufanikisha mradi huu”.
“Taarifa
tunazotuma kwa njia ya ujumbe mfupi ni pamoja na kumkumbusha mama
mjamzito tarehe za kuhudhuria kliniki, Lishe bora, , maandalizi muhimu
kabla ya kujifungua na kuwakumbusha kuhakikisha wanakwenda kujifungulia
kwenye vituo vya afya vyenye wataalam wenye ujuzi.
Napenda kuwaasa
wakina mama kujisajili kwa kupitia simu zao binafsi au kusajiliwa na
watoa huduma za afya pale wanapotembelea kliniki na hapohapo wataanza
kupokea taarifa hizi muhimu buree bila gharama yoyote. Alisisitiza Saulo
Kwa
upande wake Mkazi wa Yombo na mfanyabiashara ndogondogo Bi Mwajuma
Ally alisema “ huduma hii imekuwa muhimu sana kwangu kwani nimeweza
kupata taarifa muhimu za afya ikiwemo dalili za hatari, muda wa
kupumzika na kucheza kwa mtoto tumboni , elimu ya kumnyonyesha mtoto na
nyingine nyinge.
Mpaka sasa nimeweza kuwaunganisha kina mama wenzagu wa
3 na napenda kutoa wito kwa wa kina mama wengine kujiunga kwenye huduma
hii inayopatikana kupitia mtandao wa Airtel bila gharama yeyote. Kwa
kweli tunawashukuru sana Airtel kwa kutuwezesha sisi wamama na watoto
wadogo kuwa na afya bora wakati wote.”
Kwa
upande wake Meneja Huduma kwa jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayumi alisema
“sisi kama wadau wa huduma za mawasiliano tunatambua jinsi mawasiliano
yalivyo na mchango mkubwa katika jamii na tunajisikia furaha kuwa
mtandao wa kwanza ulioondoa gharama kwa wateja zaidi ya milioni 10
kupata taarifa hizi za afya bure bila gharama yoyote.
Lengo letu ni
kuhakikisha tunatoa fursa mbalimbali kupitia huduma za mawasiliano na
kuokoa vifo vya kinamama na watoto wachanga vinavyochangiwa na ukosefu
wa elimu ya kutosha.”
Kutokana
na mafanikio ya mpango huu sasa taarifa za afya kwa watoto hususani juu
ya lishe bora na chanjo zimeoongeza wigo kwa watoto wa hadi miaka
mitano tofauti ambapo ilikuwa hadi kwa watoto wa wiki 16. Hii itasaidia
kupunguza tatizo la utapiamlo na magonja hatarishi yanayowakumba watoto
katika umri mdogo
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.