Msanii Roma Mkatoliki
CHANZO: MUUNGWANA BLOG
Baada ya kuzagaa kwa taarifa kuhusu kukamatwa kwa Msanii Roma Mkatoliki
akiwa studio na kupelekwa kusiko julikana, Muungwana Blog imefika katika
studio za Tongwe Records jijini Dar es salaam ambapo mkasa mzima
ulikuwa hivi...
Kwa mujibu wa Mashuhuda (Majina yanahifadhiwa) walio ambao pia wanaishi
katika nyumba ambayo inapatikana studio ya Tongwe, wameijuza Muungwana
kuwa April 5, 2017 ambayo ilikuwa ni jana, katika majira ya Saa moja
jioni ilionekana gari aina ya Noah nyeusi nje ya studio hizo, ambapo
walishuka watu zaidi ya Watano na kuingia ndani ya studio hizo.
Watu hao bila ya kujitambulisha walitamka kuwa wanamuhitaji Roma na
mwenzake ambapo walimchukua na kutoka nae nje, na baada ya muda kidogo
walirejea ndani na kuwachukua wengine watano akiwemo na Prodyuza wa
studio hiyo Anayeitwa Moni.
Mbali na kuwachukua watu hao pia mashuhuda hao wemeeleza baadhi ya vifaa vya studio hiyo pia vimebebwa ikiwemo TV, na Computer.
Kwa Mujibu wa Mwanasheria wa Studio hiyo aliyejitambulisha kwa jina
moja la Edin ameiambia Muungwana Blog kuwa nikweli tukio hilo limetokea
na mpaka sasa hawajui Roma na wenzake wamepelekwa wapi na hivyo hawezi
kuelezea zaidi mpaka atakapojua walipo wakina Roma, ambapo aliongeza
kuwa anakwenda kuripoti katika kituo cha polisi cha Oysterbay Jijini
humo.
Hata hivyo saa chache baada ya tukio hilo kumekuwa na tetesi kuwa huenda
kuvamiwa kwa studio hizo kumesababishwa na nyimbo ya Tanzagiza ambayo
imeachiwa hivi karibuni na Msanii Sifa Digital ambapo mwanzoni tu wa
nyimbo hiyo linasikika jina la studio ya Tongwe Records huku maudhui ya
nyimbo hiyo yaneikashifu serikali.
Hata hivyo uongozi wa Tongwe Records umekana kuwa kuhusika na
utengezwaji wa nyimbo hiyo na kwamba msanii huyo ametumia "beat" ya
Studio hizo bila wao kujua.
Mkurugenzi wa Tongwe Records Junior Makame
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tongwe Records Junior Makame mnamo march 27, 2017 aliandika hivi kupitia ukurasa wake wa Instagram
"Sisi kama wanafamilia na uongozi mzima wa TONGWE RECORDS
tunasikitishwa na kitendo cha baadhi ya wasanii kutumia midundo/ beats /
instrumentals zetu za nyimbo zilizotoka kwa ajili ya kutengenezea
nyimbo zao za kampeni wanazozijua wao wenyewe pasipo idhini yetu..
Tunaomba ambao washafanya hivyo wazuie kusambazwa kwa nyimbo zao hizo
mara moja ili kutuepusha na lawama zitakazoletwa baada ya kufikishana
kwenye vyombo vya sheria kwa kukiuka haki zetu za kikatiba.
Wenu ktk ujenzi wa taifa
Junior ' J- Murder ' Makame. Oi"
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.