WANAJESHI wa Kenya nchini Somalia wamewauwa
wanamgambo 31 wa kundi la kigaidi la al Shabab katika shambulio
walilofanya katika kambi mbili za kundi hilo huko Jubbaland kusini mwa
Somalia. Hayo yameelezwa leo Jumatatu na jeshi la Kenya.
Nchi
hiyo ya mashariki mwa Afrika ina maelfu ya wanajeshi wake wanaohudumu
katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika huko Somalia kwa
kifupi (AMISOM).
Wanajeshi hao wa Kenya walitumwa Somalia kusaidia kuwaangamiza wanamgambo wa al Shabab na kuboresha hali ya usalama kama sehemu ya kuijenga upya Somalia baada ya kuathiriwa na vita vya ndani vya miongo miwili vilivyoidhoofisha pakubwa nchi hiyo.

Jeshi
la Ulinzi la Kenya limeeleza kuwa wanajeshi wao wa nchi kavu
walisaidiwa na helikopta na mizinga kuwashambulia al Shabab. Jeshi la
Kenya pia limefanikiwa kukamata silaha kadhaa, zana za mawasiliano na
sare za jeshi katika shambulio hilo dhidi ya kundi la kigaidi la al
Shabab huko Jubbaland.
Helikopta za Kenya katika oparesheni dhidi ya al Shabab |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.