ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 22, 2017

HII HAPA RIPOTI:- MAKONDA AKATAA KUHOJIWA NA KAMATI YA WAZIRI NAPE.

 
RIPOTI ya kamati hiyo imesomwa mbele yaWaandishi wa habari na Mwakalikishi wa kamati hiyo Deodatus Balile, Hapo chini nimekuwekea baadhi ya nukuu muhimu zilizopo kwenye taarifa hiyo ya Kamati.

"Kamati iliyoundwa na Waziri Nape kuchunguza sakata la kuvamiwa Clouds imesema kuwa RC Makonda alichagua kwa hiari kutokufanya mahojiano nao, tulienda ofisini kwake, kamati ilipopanda ngazi mkuu wa mkoa alitokea mlango mwingine na kuondoka .

Makonda alichagua mwenyewe kutosikilizwa na kamati kwa hiyo haitaathiri matokeo ya uchunguzi huu, Kamati imejiridhisha kuwa ni kweli RC Makonda alivamia kituo cha Clouds ambapo alikwenda kwa gari aliyokuwa akiendesha mwenyewe."- Balile

SIKILIZA SEHEMU YA RIPOTI.




"Chanzo cha uvamizi ni RC Makonda kutaka kurushwa kwa kipindi alichohojiwa mwanamke anayedaiwa kuzaa na Askofu Gwajima. Kamati imethibitisha kuwa Makonda na Askari aliokuwa nao waliingia mpaka kwenye ofisi za kurushia matangazo kinyume na sheria."- Balile



"Kamati imethibitisha Makonda na Askari waliovamia Clouds waliwatisha watangazaji kuwafunga miezi sita na kutuhumiwa kwa dawa za kulevya. Kutokana na vitisho hivyo, kipindi cha SHILAWADU kwa siku hiyo hakikufungwa kama utaratibu wa kipindi unavyotakiwa sababu ya vitisho."- Balile



"RC Paul Makonda aliwatishia watangazaji wa Clouds angewafunga miezi sita au kuwataja kwenye orodha ya watuhumiwa wa dawa za kulevya."- Balile

Waziri Nape amesema ripoti aliyoipokea ataiwasilisha kwenye mamlaka za juu ili wao waone ni hatua gani wanaweza kuchukua kwa RC Makonda.


 MAPENDEKEZO YA KAMATI
1.Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda awaombe radhi wafanyakazi wa kituo cha Clouds Media Groups, pia vyombo vya habari nchini kwa tukio hili la ukiukwaji wa usalama na maadili ya uandishi wa habari. 

 
2.Mhe Waziri Nape Mnauye katika kulinda maslahi ya uandishi wa habari kwa Wizara anayoiongoza awasilishe malalamiko ya wadau wa Tasnia ya Habari dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa DSM kwa mamlaka yake ya uteuzi wa mkuu huyo wa mkoa. Kuomba mamlaka ya uteuzi imchukulie hatua za kisheria zinazopaswa. 

 
3.Vyombo vya dola viwasilishe uchunguzi wa ndani juu ya askari walioingia na bunduki katika kituo cha Clouds kwa nia ya kudhibiti matukio kama haya kwa siku za usoni kwani ipo hatari ya kujengeka mazoea ya kuvamia vyombo vya utangazaji na inaweza kusababisha matatizo makubwa na usalama nchini. 

 
4.Kampuni ya Clouds Media kwa upande wake ipitie mwongozo, kanuni na sheria na taratibu zinazoongoza shughuli za utangazaji na kuangalia njia bora za udhibiti kwa watu wasio husika kuweza kuingia mara kwa mara na kufanya kazi za uhariri bila kuwa na taaluma ya habari au kuhusika katika chumba cha habari.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.