Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mazingira na Muungano), January Makmba ameahidi kukikabidhi mifuko 100 sementi Kijiji cha Katurukila kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya baada ya wanakijiji kuonyesha mwamko wa kutunza mazingira.
Akiwa katika kijiji hicho, kilichopo Tarafa ya Mang'ula Makamba alisema amefurahishwa na mwamko waliokuwa nao wakazi wa Katurukila wa kutunza mazingira bila kushurutishwa
"Hivi mnaweza kuniambia mnataka zawadi gani? Akajitokeza mwanakijiji mmoja Amir Mwema na kusema Mheshimiwa (Makamba) kituo chetu cha afya hakipo katika hali nzuri tunaomba utusaidie.
Makamba alikubali ombi hilo na kuwaahidi mifuko hiyo itakwenda Katurukila baada ya wiki moja.

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.