ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 22, 2016

TAKUKURU MWANZA YACHACHAMAA.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza, jana tarehe 21/04/2016 imemfikisha mahakamani Afisa Mtendaji wa kata ya Mwakilyambiti wilaya ya Kwimba BW. BONAVENTURA LUPILYA MAKUNGU(46) kwa kosa la kuomba hongo ya shilingi laki tatu (300,000/=) na kufanikiwa kupokea  shilingi (190,000/=) kutoka kwa JOHN MASHOMALI LUKUNGU(45).
Afisa mtendaji huyo aliomba pesa hiyo ili aweze kumpatia dhamana ndugu wa bwana JOHN MASHOMALI LUKUNGU(45), Bi  LUCIA SOBOLA JANELA ambaye yeye kama mlezi alikamatwa  kwa  kosa la utoro wa mwanafunzi LUCIA  MABULA JOHN.
Mtuhumiwa BW. BONAVENTURA LUPILYA MAKUNGU alitenda kosa hilo la kuomba na kupokea hongo mnamo tarehe 26/02/2016 ambapo ni kinyume na kifungu cha 15(1a) cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11/2007.
Mashtaka hayo yamefunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kwimba na Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU Bw. JOVINE  MAJURA ambapo yamesajiliwa kwa shauri la jinai namba 39/2016  na liko mbele ya Mheshimiwa Hakimu BONAVENTURA LEMA.
Akisomewa shauri hilo mbele ya Hakimu, Mtuhumiwa  BW. BONAVENTURA LUPILYA MAKUNGU(46) alikana shtaka hilo na yuko nje kwa dhamana  hadi shauri hilo litakapotajwa tena tarehe 24 Mei, 2016.
Wakati huohuo TAKUKURU Mkoa wa Mwanza pia inatarajia kumfikisha mahakamani Afisa Afya  na Mazingira Bw. SOSPETER JACOB SELEWA (29) wa kata ya Buswelu iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, kwa kosa la kuomba rushwa ya shilingi Laki 100,000/= kutoka kwa Bi. LYDIA JULIUS TAMBILIJA ambaye ni mmiliki wa kituo cha kulelea watoto kinachofahamika kwa jina la JITAMBUE.
Afisa Afya huyo  aliomba pesa hiyo ili aweze kufungua kituo hicho cha  kulelea watoto ambacho awali alikifunga kwa vile kituo hicho hakikuwa na baadhi ya sifa zinazostahili.



Imetolewa Tarehe 22/042016 na ERNEST MAKALE, Mkuu wa TAKUKURU(M)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.