Airtel Smartifonika yaleta simu mpya sokoni nafuu kuliko zote
Dar es salaam Octoba 22, 2015 Airtel Tanzania leo imezindua smartifoni mpya na yenye ubora zaidi ijulikanayo kama Magnus Bravo Z10 ambapo zinapatikata sasa hivi kwenye maduka yote ya Airtel nchini zikiwa zimeunganishwa na ofa ya Smartifonika inayompatia mteja muda wa maongezi wa dakika 150, 150MB na SMS 150 kwa kipindi cha miezi sita.
Akiongea na waandishi wa habari Meneja masoko wa Airtel Tanzania Aneth Muga amesema “Airtel tumekuletea Simu mpya ya Magnus Bravo Z10 ili kukuwezesha mteja wetu kuendelea kufurahia huduma zote za Airtel na zile huduma zote za kisasa za smartifoni ukiwa mahali popote
“Magnus Bravo Z10 toka Airtel inatumia laini mbili, ina radio, kioo (screen) kubwa ili kukupa raha zaidi kuona vyema unapokuwa unaitumia, pia imewekewa kamera zenye uwezo mkubwa mbele na nyuma za 5mp ili kukupa taswira au picha nzuri utakazopiga karibu au mbali ukiwa na ndugu, jamaa na marafiki” alielezea Bi Muga
“Vilevile ili uweze kufurahia huduma zote za mitandao, Airtel tumehakikisha tayari simu hii inamitandao yote ya kijamii kama facebook, Instagram, twitter na mingine mengi” . Alisema Bi Muga
Simu hii inapatikana sasa katika maduka yote ya Airtel nchini kwa gharama nafuu kuliko zote ya sh. 75,000 tu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.