ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, May 31, 2015

TUSKER YAITANGAZA “NEW JAMBO BAA” KAMA MSHINDI WA TATU WA SHINDANO LA “FANYAKWELI KIWANJANI”

Afisa Mauzo wa SBL, eneo la Manzese – Mabibo Bi. Anna Msomba, (kulia) akikabidhi baadhi ya zawadi kwa meneja baa ya “New Jambo” Bw. Frank David Lema (kulia)  baada ya baa yake kuibuka mshindi wa tatu wa  shindano la Fanya Kweli kiwanjani linaloendeshwa na Bia ya Tusker wakati wa hafla ya kuipongeza baa hiyo iliyopo Mabibo jijini Dar es salaam.
Bi.Veronika Mbilinyi (kushoto) mhudumu wa chapa ya Tusker toka SBL akikabidhi zawadi ya mfuko uliosheheni zawadi kwa Jackson Onesphory (kulia) ambaye ni mpenzi wa bia ya Tusker aliyejumuika na wengine kuipongeza baa ya wiki ya New Jambo iliyopo Mabibo jijini Dar es salaam iliyoibuka na ushindi kwenye kampeni ya Fanya kweli kiwanjani wiki hii.
Afisa mauzo wa SBL, eneo la manzese – Mabibo, Bi. Anna Msomba, (kulia) akipozi katika picha ya pamoja na wahudumu, wateja  na wafanyakazi wa Efm, wakati wa kuipongeza baa ya wiki ya “New Jambo” iliyopo Mabibo jijini Dar ambayo iliibuka mshindi wa tatu wa wiki wa kampeni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker kutoka SBL.
Ma Dj wa E-fm redio wakifanya vitu vyao  stejini ndani ya “New Jambo bar” ya  Mabibo jijini Dar es salaam wakati wa kuipongeza baa hiyo kama mshindi wa wiki wa Kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia madhubuti ya Tusker toka SBL. 
TUSKER YAITANGAZA “NEW JAMBO BAA” KAMA MSHINDI WA TATU WA SHINDANO LA “FANYAKWELI KIWANJANI”

Tarehe 30 Mei 2015, Dar es Salaam, Wadhamini wa shindano la Fanya Kweli Kiwanjani “Tusker Lager” mali ya Kampuni ya bia ya Serengeti wamemuibua mshindi wa tatu wa shindano hilo siku ya jumamosi baada ya mtanange mkali wa kuitafuta baa ya wiki uliofanywa na wadhamini hao wiki iliyopita.
“New Jambo Bar” ya Mabibo, Ubungo ndiyo iliyobahatika kuzipiga kikumbo baa nyingine 9 zilizoingia kwenye mchakato huo wa kumpata mshindi wa wiki.

Kama ilivyo ada siku ya jumamosi mameneja wa bia ya Tusker waliweka kambi katika kiwanja cha New Jambo Bar ya Mabibo jijini Dar na kuporomosha burudani ya nguvu sambamba na kugawa zawadi mbalimbali kama fulana, fedha taslim na bia za bure kwa wapenzi wa bia ya Tusker hii ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa wateja wa kinywaji hicho waliofika kupongeza ushindi wa baa hiyo.
                                  
Burudani ya kuipongeza “New Jambo Bar” kama baa ya wiki ilianza mishale ya saa kumi na moja na kudumu kwa takriban masaa sita. Burudani hiyo ya muziki ambayo ilikua ikirushwa laivu na kituo cha redio cha E-fm ni muendelezo wa sherehe mbalimbali zinazofanywa na Tusker kwenye baa mbalimbali za jiji la Dar ambazo zimeshinda shindano la “Fanya Kweli Kiwanjani”.

Akiisifia baa yake, alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari, Bw. Frank David Lema ambaye ndiye Meneja wa baa hiyo alisema “Nimefurahi sana kwa watu wa Tusker kututembelea kwenye baa yetu kwa kweli leo tumeuza kupita kiasi”. Kwa kweli natamani hata wiki ijayo wangeendelea kuichagua tena baa yetu aliongeza Meneja huyo huku akicheka na kumalizia kuwa wameuza chapa hiyo ya Tusker kuliko siku zote tangu baa hiyo ifunguliwe  kutokana na wingi wa wapenzi wa kinywaji hicho.

Kwa upande wake Afisa Mauzo wa SBL, eneo la manzese – Mabibo, Bi. Anna Msomba ambaye alikuwepo kiwanjani hapo alisema kuwa “Tumefurahi kumpata mshindi wa tatu wa shindano letu, “New Jambo baa” ni baa nzuri na ya kistaaarabu yenye wapenzi wengi wa Tusker na nadhani hii ndiyo sababu kubwa ya watu kuipigia kura baa hii…Kampeni hii bado inaendelea na tunatarajia zaidi ya baa 20 kuingia kwenye kinyang’anyiro hiki kabla ya promosheni kufikia tamati”.

Bi. Msomba aliendelea kuwasihi wadau na wapenzi wa bia ya Tusker kuendelea kuzipigia kura baa mbalimbali zitakazo orodheshwa kwenye shindano hilo na kukumbushia kuwa ili kuziwezesha baa za mitaa tunayoishi kuingia kwenye shindano hili wasisite kusikiliza kipindi cha Ubaoni cha E-fm ambacho kinadadavua kwa undani kuhusiana na promosheni hiyo.


Pamoja na hayo, Meneja huyo alikabidhi Tsh. 100,000Tsh fedha taslim kwa wahudumu wa baa hiyo kama zawadi kwa kufanya kweli kwenye upande wa kutoa huduma kwa siku hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.