|
Mwakilishi wa kampuni ya Airtel mkoa wa shinyanga Ezekiel Nungwi (kushoto) akimpa mkono wa pole mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akipokea mara baada ya kukabidhi misaada ya vitu mbali mbali na kutoa pole kwa wathilika wa mvua za mawe ambapo zilitokea tarehe 3 usiku mwezi katika kijiji cha mwakata na kupoteza maisha ya watu 46 na majeruhi zaidi 96 na wengi kuvujika miguu na mikono katika tukio hilo |
|
Baadhi ya Vitu mbali mbali kutoka kampuni ya simu ya Airtel kwa wathilika wa maafa katika kijiji cha mwakata ambapo kampuni hiyo ya Airtel imetoa,sabuni ,mabati ,maharange ,mchele ,mafuta. |
|
Mary Machibya wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Wakiwafariji wathilika wa mvua ya mawe |
|
Jinsi maafa hayo yalivyotokea na kuharibu miundombinu ya makazi. |
|
Hali tete. |
|
Kutoka maisha ya nyumba halisi hadi banda hakika ni maisha magumu. |
|
Kaya hii nayo imeathiriwa. |
|
Moja kati ya nyumba zilizobomolewa na mvua iliyonyesha hivi karibuni wilayani Kahama. |
|
Hali halisi na jinsi maafa hayo yalivyotokea na kuteketeza nyumba za baadhi ya kaya mifugo na mali mbalimbali. |
|
Mama Ndallo Charles muathilika wa mvua ya mawe . |
|
Joseph Maganga akiongelea jinsi maafa hayo yalivyotokea na kupoteza mifugo yake yote mbuzi 52 na kuku kumi 10 katika yukio hilo |
Airtel yatoa msaada kwa wahanga wa mafuriko Kahama
·Yazindua namba kwa wateja wake kuchangia kwa kutuma ujumbe kwenda namba 15626
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imetembelea wahanga wa mfuriko ya mvua katika wilaya ya kahama mkoani shinyanga kwa kuwapatia msaada wa mahitaji muhimu yanayoitajika kwa sasa. Zaidi ya watu 35 walifariki na kuwaacha mamia wakiwa hawana makazi ya kukaa kufatia mvua kubwa iliyonyesha mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu
Akionge wakati wa makabithiano ya msaada huu, Meneja mauzo wa Airtel Shinyanga Bwana Ezekiel Nungwi alisema” Tunaungana kwa pamoja katika maafa haya na kutoa pole kwa familia zilizopoteza marafiki na wanafamilia kutokana na mafuriko haya.
Tunatambua pia mafuriko haya yamewaacha wakazi wengi bila makazi, huku mazao yao kuharibiwa na mifugo yao kufa hivyo tunaungana kwa pamoja kutoa msaada kwa namna tutakayoweza . Leo kwa niaba ya Ofisi yetu ya kanda ya Shinyanga tunatoa msaada wa mabati, mablanketi, magodoro pamoja na chakula vyenye thamani ya shilingi milioni 3 na kuwaomba watanzania kuungana nasi kuwasaidia ndugu zetu wa kahama ili kuepuka milipuko ya magonjwa isitokee na kuwawezesha kurudi kufanya shughuli zao za kawaida mapema iwezekanavyo.
Sambamba na mchango huu, tunapenda kuzindua namba maalumu itakayowawezesha watanzania kuchangia. Tunachukua fulsa hii kuwaomba wateja wetu kuchangia kwa kutuma ujumbe wenye neno MAAFA kwenda namba 15626 , ujumbe huu utalipiwa shiling 256 na pesa hiyo itaingia kwenye mfuko wa kuchangia wahanga wa mafuriko mkoani Shinyanga,
Akiongea kwa niaba ya wakazi wa Kahama helen Benjamin Alisema” Tunawashukuru sana Airtel kwa msaada huu ulikuja wakati tunauhitaji zaidi, Tunawashukuru kwa kuanzisha namba itakayowapa fulsa watanzania kuchangia, napenda kuwaomba watanzania kushiriki kwa kuchagia na kwa makampuni mengine kujitolea na kutusaidia katika hali ngumu ambayo imetuweka kwenye hatari kupata milipuko ya magojwa na zaidi tumekosa makazi na shughuli zetu za kiuchumi zimeteketea. Tunawashukuru waliojitolea mpaka sasa na tunaomba muendelea na moyo huo wa kujitolea.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.