ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 10, 2013

SUPER D YUKO JIJINI MWANZA: KUFANYA ZIARA YA KUHAMASISHA NGUMI MIKOA 16


SUPER D AKIWA NA VIFAA VYAKE VYA KUFUNDISHIA MASUMBWI


KOCHA wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' yupo katika ziara ya kutembelea mikoa mbalimbali hapa nchini tangia mwishoni mwa mwezi uliopita ambapo mpaka sasa katika ziara yake hiyo kesha tembelea mikoa kadhaa ya Tanzania Bara akianzia na Tanga,Moshi,,Arusha,Karatu,Babati Mwanza ,Shinyanga na Kahama

Ziara hiyo yenye lengo la kuhamasisha mchezo wa ngumi kwa vijana na kuwapa mbinu mpya baadhi ya makocha wa mikoa husika ili mchezo wa ngumi uweze kusonga mbele ingawa mchezo huo unapendwa na wenga na kukwepwa na wadhamini ndicho kitu kinachokifanya mchezo wa masumbwi uonekane umeshuka hadhi yake wakati bado upo juu

Akizungumzia safari hiyo Super D '' Amesema safari hiyo ni ya manufaa sana kwa watu wa mikoani kwani bado mikoa mingi atatembelea kutoa elimu ya mchezo huo na kuhamasisha vijana wengi wajiunge na mchezo huo kwani yaweza kuwa ni ajira yao 

SUPER D akiwa MWANZA

Super D ambaye ni kocha wa kwanza kutoa mafunzo yake kwa njia ya DVD zilizochanganywa na clips mbalimbali

CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa ali ya juu ambazo ni chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi

DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani wasiliana na kocha kwa simu 0713406938 ili uweze kupata dvd hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi mchezo huo

DVD zina mabondia wakari wanaotamba Duniani kama vile Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali 
na wengine wengi 

Super D aliongeza kuwa mikoa mingine atakayotembelea ni Tabora, Singida, Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya na Songea ambapo amewaomba baadhi ya makocha, wadau wa mchezo huo wa mikoa husika ambao ajawai kuonana  mikoa iliyotajwa kuwasiliana nae ili wabadilishane ujuzi kwani kuna wengine hawana mawasiliano nao waweza kumpigia kwa 0713 406938 ili kupeana ufundi na ujuzi zaidi wa mchezo wa masumbwi ili usonge mbele  zaidi

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.