ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 10, 2013

MANISPAA YA ILALA YAFANYA ZIARA JIJINI MWANZA NIA KUBADILISHANA UZOEFU

Mtahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (kulia) akimkaribisha Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry William Silaa katika ofisi za jiji la Mwanza kwaajili ya kujadili masuala mbalimbali ya Ushirikiano pamoja na kubadilishana uzoefu katika masuala ya utendaji, kuihudumia jamii pamoja na suala la usafi.


Awali Meya wa Ilala Jerry Silaa alipata fursa ya kusaini kitabu cha wageni. 


Msemaji jiji Dr.Kaaya (aliyesimama) akitoa utambulisho ndani ya ofisi za Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Hida Hassan (aliyeketi mbele) kwa wageni toka Manispaa ya Ilala waliopo jijini Mwanza kwaajili ya ziara ya kubadilishana uzoefu na ofisi za Halmashauri ya jiji la Mwanza.


Wageni hawa toka Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam ni viongozi madiwani na wakuu wa idara nyeti katika ofisi za Manispaa. 


Engo nyingine ya wageni.
Eh bana eeeh...Hizi ndizo tuzo mbalimbali zilizopo ndani ya ofisi za jiji la Mwanza.


Afisa Uhusiano wa jiji la Mwanza Joseph Mlinzi akitoa malezo juu ya Historia ya jiji la Mwanza, changamoto na harakati zake za shughuli mbalimbaliza kimaendeleo.


Kila kitengo kilitoa maelezo juu ya utendaji wake na kisha maswali yakapata nafasi yake.


 Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa (kushoto) akimkabidhi bao la kisasa Mstahiki meya wa jiji la Mwanza kama zawadi ya ushirikiano kwa Majiji hayo.


'Mgeni njoomwenyeji apone'  Naye Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Hida Hassan alikabidhiwa zawadi ya 'kibenki cha kuhifadhi fedha kama ishara ya kuwa mwaminifu na suala la mapato na matumizi ya fedha kwa ofisi yake anayoitumikia.


Sasa ni picha ya pamoja kwa majiji dada Mwanza na Ilala.


Picha ya pamoja Ilala na Meya Jerry Silaa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.