ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, April 7, 2026

NI ZAIDI YA NUSU KARNE SASA TANGU MAUAJI YA KARUME.

 


🏴Leo ni kumbukizi ya miaka 54 tangu kuuawa kwa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, kiongozi aliyebeba alama ya mapambano, mageuzi na ujenzi wa taifa jipya visiwani humo.


Karume aliuawa Aprili 7, 1972, kwa kupigwa risasi katika eneo la Kisiwandui, Unguja, yalipokuwa Makao Makuu ya Chama cha Afro-Shiraz. Tukio hilo liliacha pengo kubwa katika uongozi wa Zanzibar na historia ya siasa za Tanzania kwa ujumla.

Miaka zaidi ya nusu karne baadaye, wadau wa siasa na wananchi kwa ujumla wanaendelea kumkumbuka kwa misingi aliyoiasisi ikiwemo msisitizo wa usawa wa kijamii, uzalendo, na ujenzi wa uchumi unaowajali wananchi wa kawaida. Hata hivyo, baadhi yao wanahoji kuwa dira na maono hayo yameanza kufifia au kupuuzwa kadri nyakati zinavyobadilika.

Kumbukizi hii si tu ya kuenzi maisha yake, bali pia ni fursa ya kutafakari juu ya misingi aliyosimamia, na kujiuliza kama bado ina nafasi katika kuongoza maendeleo ya Zanzibar ya leo.
.
.
#KarumeDay

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment