ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 21, 2022

SHAHIDI AELEZA WALIVYOWAKAMATA WATUHUMIWA KESI YA KINA MBOWE.

 


CHANZO:- MWANANCHI
Shahidi wa 11 upande wa mashtaka katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu ameieleza mahakama alivyoshiriki katika kuwakamata na kuwasafirisha hadi Dar es Salaam watuhumiwa katika kesi hiyo.


Akitoa ushahidi wake leo Ijumaa Januari 21, 2022 Askari mpelelezi Sajenti Goodluck ameleza alivyomkamata mtuhumiwa mwingine aitwaye Halfan Bwire maeneo ya Polisi Chang'ombe Jijini Dar es Salaam.


Soma ushahidi wote hapa


Wakili Kidando: Mheshimiwa Jaji shauri hili linakuja kwa anili ya kusikilizwa kwa leo tuna shahidi mmoja tuko tayati kuendelea


Jaji: Utetezi?


Kibatala: Nasi tuko tayari


shahidi ameitwa na anapanda kizimbani


Jaji: Majina yako


Shahidi: Naitwa H.4347 Detective  Sajent Goodluck


Jaji: Umri wako


Shahidi: miaka 32


Jaji: Dini


Shahidi: Mkristo


Jaji: Kabila lako?


Shahidi:Mchaga


Shahidi anaongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Pius Hilla.


Shahidi: Naitwa Detective Sajent Goodluck


Soma zaidi: Kesi ya kina Mbowe kuanza na kiporo cha mapingamizi


Kazi yangu ni Askari Polisi tangu mwaka 2013 na kituo changu cha kazi ni Central Police Arusha, niko hapo tangu mwaka 2014.


Jukumu langu ni Upelelezi wa Makosa ya jinai.


Shahidi: Tarehe 4/8/2020 nilikuwa kazini Polisi Arusha, nikiendelea na majukumu yangu, jioni siku hiyo nilipata taarifa kutoka kwa afande Mahita kuwa tunahitajika kwa Afande RCO, (Mkuu wa Upelelezi mkoa) mimi na Koplo Francis.


Shahidi: Afande Mahita ni Msaidizi wa Afande OC-CID (Mkuu wa Upelelezi Wilaya).


Shahidi: Aliyekuwa RCO kipindi hicho alikuwa ni Afande Ramadhani Kingai


Shahidi: Tulipofika kwa Afande RCO alisema kuwa kuna kazi ya kufanya.


Shahidi: Mimi na Koplo Francis tulikwenda kuchukua silaha, Mimi nilichukua AK47 na mwenzangu pia.


Shahidi: Baada ya kuchukua silaha tulirudi mkoani kwa Afande RCO. Alisema tunatakiwa twende Polisi Usa River Wilaya ya Arumeru.


Shahidi: Muda huo ilikuwa Ni majira ya saa 12 jioni


Shahidi: Safari ya kuslekwa Usa Riva ilihusisha Afande RCO,Mimi, Afande. Mahita, na Koplo Francis.


Shahidi: Baada ya kufika kituo Polisi Usa River tuliingia kituoni tukamkuta OC- CID ambaye alikuwa ni Afande Jumanne. Alikuwa nje ya kituo.


Shahidi: Alitukaribisha ofisini kwake ambapo wote tuliingia.


Shahidi: Tukiwa ofisini Afande RCO alitwambia amepewa maelekezo ya kuandaa timu ya kufanya kazi ambayo ni kazi maalum.


Shahidi: Hakusema alipewa maelekezo na nani.


Shahidi: Alitwambia kuwa amepata taarifa kuna kitu cha watu wamekula njama kufanya vitendo vya kigaidi maeneo mbalimbali.


Soma zaidi:Shahidi augua, kesi ya kina Mbowe yaahirishwa


Shahidi: Alitwambia pia taarifa alizozipata kikundi hicho kuna watu wako Kilimanjaro Moshi.


Shahidi: Kwamba kikundi hicho kimepanga kuwadhuru viongozi akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, na kufanya maandamano yasiyokuwa na kikomo.


Shahidi: Pia alitueleza kuwa kikundi hicho kinaratibiwa na mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe.


Shahidi: Afande Kingai alitwambia kuwa kikundi hicho kimepanga kuchoma vituo vya mafuta na kukata miti magogo kupanga barabarani, ili kuleta tahauruki kwa Wananchi, nchi ionekane haitawaliki


Shahidi: Afande Kingai alitwambia kwamba kwa taarifa alizonazo kuna wengine tayari wako Moshi kwa hiyo tunatakiwa twende Moshi ili kuzuia uhalifu huo usifanyike.


Shahidi: Afande Kingai alitwambia tunatakiwa tuwakamate.


Shahidi: Baada ya maelekezo hayo tuliondoka kuelekwa Moshi.


Shahidi: Safari ya kuelekea Moshi ilihusisha Afande RCO Kingai, Afande Jumanne, Afande Mahita, Koplo Francis pamoja na DC Azoz, here wa Afande RCO.


Shahidi: Baada ya kufika Moshi, tulienda maeneo ya Central Police Moshi.


Shahidi: Afande Kingai alishuka kwenye gari akawa anafanya mawasiliano, baada ya hapo tulienda kuzunguka mjini ili kuwakamata wahalifu hao.


Shahidi: Kazi yetu kwa siku hiyo ilikuwa ni kuwatafuta wahalifu lakini hatukufanikiwa kuwakamata. Tulifanya hivyo hadi majira ya saa tano usiku.


Shahidi: Ilipofika majira ya saa tano kuelekea saa sita, Afande Kingai alisema kwa kuwa hatukufanikiwa kuwakamata kwa taarifa alizokuwa anazipokea yeye alisema tukapumzike.


Shahidi: Tarehe 5 asubuhi Afande Kingai alikuwa anaendelea kupokea taarifa kutoka kwa mtu aliyekuwa anampa taarifa na mpaka majira ya saa sita kuelekea saa saba ndipo Afande Kingai alisema amepata taarifa mahali walipo. Alionyesha mwonekano wao kisha akatuambia tuondoke twende eneo la Rau Madukani.


Shahidi: Kulikuwa na watuhumiwa watatu.


Shahidi: Baada ya Afande Kingai kutueleza hivyo tuliondoka kuelekea maeneo ya Rau Madukani kwa ajili ya kuwakamata wahalifu.


Shahidi: Baada ya kufika Rau Madukani, tulipaki gari na Afande Kingai akampa maelekezo Afande Mahita ashuke kwenye gari aende kuangalia mahali walipokuwa.


Shahidi: Afande Mahita alishuka kwenye gari akaenda kuangalia.


Shahidi: Haikuchukua muda mrefu Afande Mahita alirudi akatwambia kwamba nimewaona wote watatu wamekaa kwenye grocery.


Shahidi: Baada ya taarifa hiyo ya Afande Mahita, Afande Kingai akatoa maelekezo ili twende kuwakamata watuhumiwa. Afande Kingai aligawa timu mbili, moja iliongozwa na Afande Kingai. Afande Jumanne na mimi na nyingine ilikuwa inaongozwa na Afande Mahita, Mimi na Koplo Francis na dereva alibaki kwenye gari.


Shahidi: Timu moja ambayo nilikuwepo mimi ikiongozwa na afande Kingai ilipita kulia na timu ya Afande Mahita ilipita kushoto.


Shahidi: Baada ya Afande Kingai kuwa na timu mbili tulielekea eneo la tukio kwenywe grocery.


Shahidi: Kabla ya sisi kufika kwenye grocery nilisikia sauti ya Afande Mahita akiwaweka watu chini ya ulinzi.


Shahidi: Baada ya kusikia sauti tuliongeza mwendo kuelekea eneo la tukio, tulimkuta Afande  Mahita na Koplo Francis amewaweka watu wawili chini ya ulinzi.


Shahidi: Baada ya kufika mahali walipokuwa watuhumiwa Afande Kingai alijitambulisha kwa watuhumiwa. Baada ya kujitambuliaha aliwauliza watuhumiwa majina yao.


Shahidi: Mtuhumiwa wa kwanza alijitambulisha kwa kina la Adamu Kasekwa na mtuhumiwa mwingine akijitambulisha kwa jina la Mohamed Ling'wenya.


Shahidi: Baada ya utambulisho huo, Afande Kingai alimpa maelekezo Afande Jumanne kuwapekuwa watuhumiwa.


Shahidi: Wakati huo mimi na Koplo Francis tulikuwa tumeimarisha ulinzi.


Shahidi: Afande Jumanne aliwaita mashahidi wawili waliokuwepo karibu, mmoja alikuwa anauza grocery na mwingine alikuwa kwenye bar, mmoja anaitwa Ester na mwingine anaitwa Anitha.


Shahidi: Baada ya mashahidi kufika Afande Jumanne alianza kumpekua mtuhumiwa wa kwanza.


Shahidi: Mtuhumiwa wa kwanza aliyeanza kupekuliwa ni Adamu Kasekwa.


Shahidi: Baada ya kugeuka alianza kumpapasa kuanzia juu alipofika kiunoni alitoa bastola, upande wa kushoto.


Shahidi: Baada ya kutoa bastola aliinyoosha juu kwa mashahidi, akasoma namba zilizokuwa kwenywe bastola A5340. Alisoma jina la ile silaha. Alisema ni Luger.


Shahidi: Baada ya hapo alitoa magazine akahesabu risasi zilizokuwemo.


Shahidi: Risasi alizozitoa kwenye magazine aliIhesabu zilikuwa ni tatu.


Shahidi: Baada ya hapo aliendelea kumpekua mtuhumiwa akatoa kikaratasi ambacho kilikuwa nadawa zinazodhaniwa za kulevya kwenye mfuko wa suruali.


Shahidi: Ile bastola alinikabidhi na zile kete pia alinikabidhi


Shahidi: Afande Jumanne aliendelea kumpekua mtuhumiwa wa pili ambapo alimkuta mfuko na simu aina ya Itel. Alitoa betri akasoma namba za simu. Baada ya kumpekua akiamuru mtuhumiwa akae chini na akinikabidhi ile simu.


Shahidi: Baada ya hapo Afande Jumanne aliniambia nichukue bahasha kwenye gari. Kwa sababu gari ilikuwa imesogea eneo la tukio nilichukua bahasha nikamkabidhi akatoa document kwa ajili ya kujaza.


Shahidi: Baada ya kumkabidhi Afande Jumanne ile bahasha akitoa karatasi akaanza kujaza vile vielelezo kwenye hati ya kukamatia mali.


Shahidi: Nakumbuka alijaza hati mbili. Hati ya kwanza alijaza silaha na zile simu, hati nyingine alijaza madawa yadhaniwayo kuwa ya kulevya.


Shahidi: Baada ya kumaliza kujaza vielelezo, alisaini afande Jumanne, wakasaini mashahidi pamoja na watuhumiwa


Shahidi: Baada ya hapo alimuamuru mtuhumiwa akae chini na alimuamuru mtuhumiwa wa Pili asimame, ni Mohamed Ling'wenya.


Shahidi: Baada ya kumuamuru mtuhumiwa wa pili asimame akamuamuru ageuke na baada ya kugeuka alimpekua kwa kumpapasa kuanzia kichwani, alipofika mfukoni alitoa kete zinazodhaniwa kuwa dawa za kulevya.  


Shahidi: Hizo kete zilikuwa kwenye kimfuko kama paketi za karanga, akizihesabu mbele ya mashahidi na vilikuwa 25.


Shahidi: Baada ya hapo alinipa nizishike. Aliendelea kumpekua mtuhumiwa ambapo alimkuta na simu moja aina ya  Tecno, ilikuwa kwenye mfuko wa suruali.


Shahidi: Alitoa betri akasoma IMEI number na akasoma namba za ile line na akajaza hati ya kukamatia mali vielelezo hivyo. Afande Jumanne alisaini, mashahidi walisaini pamoja na mtuhumiwa mwenyewe alisaini.


Shahidi: Baada ya Afande Jumanne kujaza hati zote za ukamataji mali vile vielelezo nilipewa Mimi. Afande Kingai alielekeza tuelekee kwenye gari baada ya kufika Afande Jumanne aliandaa hati ya makabidhiano ya vielelezo ambayo alikuwa ameiandaa yeye akanikabidhi Mimi pamoja na silaha na simu.


Shahidi: Hati niliyokabidhiana silaha na Jumanne nitaitambua kwa sababu ina jina langu, H4347 Detective Goodluck jina la aliyenikabidhi, Afande Jumanne na vielelezo nilivyokabidhiwa


Shahidi: Wakili anamuonesha nyaraka na anamuuliza Ni nyarakangani na shahidi anajibu.


Shahidi: Ni hati ya makabidhiano mali. Nimeitambua kwa saini yangu, majina yangu, tarehe ya makabidhiano 5/8/200/2020 na vielelezo nivyokabidhiwa.


Shahidi: Kwa mujibu wa hati anayekabidhi ni Afande Jumanne, anayekabidhiwa ni nini H4347 Detective Goodluck.


Shahidi: Kinachokabidhiwa ni bastola aina ya Luger.


Shahidi: Makabidhiano yalifanyika tarehe 5/8/2020.


Shahidi: Baada ya kuitambua hati hiyo wakili Hilla anairejesha kwa karani hati hiyo na anaendelea kumuongoza shahidi.


Shahidi: Baada ya makabidhiano hayo tuliondoka kuelekea kituo cha Polisi Moshi, tukiwa na Afande Kingai, Afande Jumanne, Afande Mahita, Mimi na watuhumiwa Adamu Kasekwa na Mohamed Ling'wenya.


Shahidi: Tulikuwa kwenye gari la Afande Kingai


Shahidi: Koplo Francis alikuwa kwenye gari lingine la RPC Arusha pamoja na mashahidi huru.


Shahidi: Tukiwa tunaelekea kituoni, Afande Kingai aliuliza taarifa tulizo nazo mko watatu mwingine yuko wapi? Watuhumiwa wenyewe wakasema kuwa kweli lakini hawajui mwenzao ameenda wapi  


Shahidi: Kituoni Afande Jumanne walishuka lakini Mimi na Afande Kingai hatukushuka pamoja na watuhumiwa sababu Afande Kingai alisema kuwa tunatakiwa kwenda kumtafuta mtuhumiwa mwingine.


Shahidi: Waliporejea akina Afande Jumanne tuliondoka kwenda kumtafuta mtuhumiwa kwa sababu watuhumiwa walisema atakuwa maeneo ya karibu.


Shahidi: Baada ya kufika eneo la tukio hatukufanikiwa kumkamata lakini watuhumiwa wenyewe walionesha nia ya kusaidia kumpata.


Shahidi: Baada ya kutueleza hivyo, tulichukua hatua ya kuzunguka katika maeneo ambayo watuhumiwa walituongoza.


Shahidi: Walimtaja kwa jina la Lujenge.


Shahidi: Ufuatiliaji wa siku hiyo hatukufanikiwa kumkamata mpaka majira ya saa tano.


Shahidi: Baada ya kutokumkamata mtuhumiwa Afande Kingai alisema kuwa ni wa kuwarudisha watuhumiwa kituoni wakawekwe lockup


Shahidi: Baada ya watuhumiwa kuwekwa lockup tulirudi na kuendelea na ufuatiliaji.


Shahidi: Afande Kingai ndio alikuwa anafanya mawasiliano.


Shahidi: Tarehe 6 /8/2020 majira ya asubuhi saa 11 tukifika kituoni tukawachukua watuhumiwa kwa madhumuni ya ufuatiliaji mtuhumiwa.


Shahidi: Tulienda maeneo mbalimbali Moshi, kama Machame mpaka Aisho Hoteli


Shahidi: Mbali na maeneo hayo pia tulienda Sakina, hatukufanikiwa tukarudi Moshi Police. Afande Kingai akapata maelekezo kwamba watuhumiwa wanatakiwa wapelekwa Dar es Salaam.


Shahidi: Baada kutoka Central Moshi tulipofika njiapanda ya Himo gari ikapata hitilafu, Afande Kingai alifanya mawasiliano ya kupata gari nyingine.  


Shahidi: Baada ya hapo wakati tunasubiria kupata gari nyingine kutoka Moshi Afande Kingai alikuja na chakula, alikuwa amebeba ndizi na nyama tukala


Shahidi: Gari ilitoka Moshi. Baada ya gari ya RPC Moshi kufika tuliwahamisha watuhumiwa tukaendelea na  safari.


Shahidi: Tulifika Dar es Salaam tarehe 7/8/2020 saa 11 alfajiri. Watuhumiwa walikabidhiwa charge room.


Shahidi: Baada ya kukabidhi watuhumiwa Afande Kingai alielekeza tuondoke ili tukanawe uso baada ya hapo turudi saa moja.


Shahidi: Baada ya kurudi kituoni Afande Kingai alinielekeza nikabidhi vielelezo.


Shahidi: Maelekezo hayo niliyatekeleza nilikwenda kwa mtunza vielelezo, nikakabidhi silahà namba A5340.


Shahidi: Nilimkabidhi St/Sgt Nuru.


Shahidi: Muda wote huo silaha nilikuwa nayo kwenye begi.


Shahidi: Vingine nilivyokabidhi ni simu, simu nilimkabidhi Afande Swila, ni Askari wa hapa Dar es Salaam. Nilimkabidhi simu tulizokamata kwa watuhumiwa kule Moshi aina ya Tecno na Itel pamoja na line.


Shahidi: Baada ya kukabidhi vielelezo Afande Kingai akielekeza kuwa tuendelee na ufuatiliaji ni wa taarifa ambazo alizokuwa anazipata na kwamba tuungane na Afande Swila.


Shahidi: Makabidhiano ya vielelezo tulikabidhiana kwa kusaini hati ya makabidhiano. Ilikuwa ni tarehe 7/8/2020.


Shahidi: Hiyo hati ya makabidhiano ya silaha, risasi naweza kuitambua kwa majina yangu, tarehe ya makabidhiano, vielelezo ambavyo tulitoka navyo Moshi pia na jina la mkabidhiwa.


Shahidi: Wakili Hilla anamuonesha shahidi hati ya makabidhiano ya vielelezo na shahidia anasema anaitambua kuwa ndio hati ya makabidhiano aliyoijaza wakati akimkabidhi Sajent Nuru vielelezo.


Shahidi: Naiomba mahakama ipokee kama ushahidi.


Mawaili wa utetezi wanaikagua.




Mawakili wote Nashon Nkungu ( kwa mshtakiwa wa kwanza), John Mallya (kwa mshtakiwa wa Pili), Fredrick Kihwelu ( kwa mshtaiwa wa tatu) na Kibatala kwa mshtakiwa wa nne wanaeleza kuwa hawana pingamizi.


Mahakama imeipokea hati hiyo ya makabidhiano mali baina ya shahidi na Sajenti Nuru kuwa kielelezo cha 36 cha ushahidi wa upande wa mashtaka.


Kisha shahidi anasoma maelezo yaliyomo kwenye Katika hati hiyo ya makabidhiano ya mali


Shahidi: Tarehe 8/8/2020 tulikuwa tunaendela na ufuatiliajibwa watuhumiwa wengine walioko Dar Afande Kingai akituelekeza mimi na Afslande Mahita kuwahamisha watuhumiwa kutoka Police Central kwenda kituo cha Polisi Mbweni, ilikuwa muda wa saa 5 asubuhi. Watuhumiwa tuliowahamisha kutoka Central kwenda Polisi Mbweni ni wstujumiwa tuliotoka nao Moshi ambao ni Adamu Kasekwa na Mohamed Ling'wenya.


Shahidi: Tuliohusika kuwahamisha Ni Afande Jumanne, Afsnde Mahita, Arande Swila pamoja na mimi na dereva.


Shahidi: Baada ya kufika Polisi Mbweni tulishuka na watuhumiwa, chargeroom (chumba cha mashtaka) wakiingia na Afande Jumanne na Afande Mahita kuwakabidhi watuhumiwa.


Shahidi: Baada ya watuhumiwa kukabidhiwa tuliondoka kufuatilia taarifa mbalimbali kuhusiana na watuhumiwa wengine.


Shahidi: 9/8/2020, tulikuwa tunafuatilia taarifa zilizokuwa zinatolewa, tukiwa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam..


Shahidi: Siku hiyo maeneo ya jioni nilikuwa maeneo ya Temeke.


Shahidi: Siku hiyo ya terehe 9 nilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mwingine aitwaye Halfan Bwire. Bwire alimamatiwa maeneo ya Polisi Chang'ombe.


Shahidi: Mazingira ya ukamataji wa Bwire, alikuwa kwenye gari ya abiria daladala, kwa hiyo ilielekezwa kuingia kituo cha Polisi Chang'ombe.


Shahidi: Baada ya gari kuingia kituoni, Mimi na Afande Mahita tulielekezwa kuongia kwenye gari ndipo tukamkamata.


Shahidi: Kwenye upekuzi wa mtuhumiwa tulimkuta na simu mbili, mfukoni katika suruali ya mtuhumiwa.


Shahidi: Baada ya upekuzi mtuhumiwa aliingizwa lockup kituo cha Polisi Chang'ombe.


Shahidi: Sisi Tuliendelea na ufuatiliaji wa taarifa nyingine ambazo tulikuwa nazo.


Wakili Hilla: Mheshimiwa Jaji tunaomba ahirisho kwa ajili health break.


Kibatala: Mheshimiwa, hatujui amebakiza maelezo marefu kiasi gani kama si ndefu tungeomba angemaliza.


Hilla: Mheshimiwa Jaji bado tuna mambo mengi hatuwezi kukadiria muda.


Jaji: Tuna-break mpaka saa 7:45.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.