MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Kundi la Asasi za Kiraia NGOs Tanzania Bara, Mhe Neema Lugangira kulia akiagana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Zainabu Chaula leo Jumatatu 24 Januari 2022, katika Ofisi za Wizara iliyopo Mji wa Magufuli, Mtumba, Dodoma mara baada ya kufanya mazungumzo naye
NA MWANDISHI WETU, DODOMA
NA MWANDISHI WETU, DODOMA
MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Kundi la Asasi za Kiraia NGOs Tanzania Bara, Mhe Neema Lugangira amewasilisha mapendekezo ya maeneo ambayo yanayohitaji kufanyiwa Maboresho ili kuimarisha Ustawi wa NGOs hapa Nchini.
Mbunge Neema aliwasilisha mapendekezo hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Zainabu Chaula leo Jumatatu 24 Januari 2022, katika Ofisi za Wizara iliyopo Mji wa Magufuli, Mtumba, Dodoma.
Alisema mambo hayo yanahitaji kufanyiwa kazi kwa mwaka huu 2022 ambayo ni pamoja na kuandaa Mpango wa Kuwajengea Uwezo NGOs za Mikoani ili waweze kujiendesha kwa Mujibu wa Sheria.
Mbunge huyo alisema suala lingine ambalo walilizungumza ni kuandaa Mikutano ya Kimkakati na Wadau wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika maeneo mahsusi ikiwemo Maboresho ya Kanuni za Usimamizi wa Fedha za NGOs
Alisema Maboresho mengine aliyowasilisha ni katika Kodi kwa Wafanyakazi Wanaojitolea
(Volunteers) na Maboresho ya Kodi ya Mapato (Income Tax) kwa Kundi hili la NGOs.
Hata hivyo Mbunge Neema Lugangira aliwasilisha shukrani kutoka Sekta ya Azaki (NGOs) kwenda kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujibu kilio cha muda mrefu na kuunda Wizara Mpya inayosimamia Masuala ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na Sekta ipo tayari kushirikiana kwa karibu na Wizara hii muhimu.
Katika hatua nyengine Mbunge Neema Lugangira alimpongeza sana Dkt. Zainab Chaula kwa Kuteuliwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kuwaKatibu Mkuu wa Wizara hii mpya na muhimu sana.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii Dkt. Zainab Chaula amuhakikishia Mbunge huyo kuwa Ofisi yake ipo wazi kwa ajili ya majadiliano na kubadilishana mawazo hivyo anawakaribisha sana Wadau wa Sekta ya NGOs ili kwa pamoja walete mageuzi ya kimaendeleo katika Masuala yote ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
Dkt Chaula amewahikikisha Sekta ya NGOs atashirikiana nao kwa karibu ili kwa pamoja waweze Kuimarisha Mazingira Wezeshi kwa Ustawi wa NGOs ambao ni Wadau muhimu katika Utekelezaji wa Mipango ya Wizara yake.
Kwa kuhitimisha, Dkt. Zainab Chaula, Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumy amesisitiza kuwa Ofisi yake ipo wazi kwa ajili ya majadiliano na kubadilishana mawazo hivyo anawakaribisha sana Wadau wa Sekta ya NGOs.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.