Onyo: makala hii inaambatana na picha ambazo zinaweza kuumiza hisia za baadhi ya wasomaji.
Wakati unapoingia makaburi ya Pomuch kwa mara ya kwanza, huenda ukahisi kuwa na wasi wasi na hata kuogopa, ukiamini kuwa unatazamwa na mafuvu ya vichwa. Licha kuwa kwa zile dakika chache za kuzuru eneo hili, mtu anayetembea kupitia njia nyembamba za mababuri haya hushikwa hata na hofu zaidi ya kutaka kugeuza, wakati mwingine kuangusha baadhi ya masanduku yaliyo na mifupa ya maiti.
Katika mji huu ulio jimbo la Campeche kusini mashariki mwa Mexico , mifupa hii ya watu habaki eneo hili kwa mwaka mzima kwa masanduku. Hata hivyo ni wakati huu wa mwaka, muda mfupi kabla ya siku ya wafu ambapo majirani zake hufanya utamaduni unaowavutia mamia ya watalii, utalii ambao ni wa kusafisha mifupa ya jamaa zao waliofariki.
Tambiko hilo ambalo kwa lugha ya Maya linafahamika kama Choo Ba'ak limesherehekewa mjini huko kwa takriban miaka 150, kulingana na Hernesto Pool, anayeunga mkono utamaduni huo. "Tunafuata utaratibu wa Maya, unaosema kuwa wafu walikuwa na maisha zaidi. Kwa utamaduni huu wa kuabudu wafu, tunaelewa kuwa kuna maisha baada ya kifo," anaiambia BBC.
Usafishaji mifupa ya watu
Makaburi ya Pomuch yanamilikiwa na manispaa ya Hecelchakán, eneo lenye joto na tulivu katika rasi ya Yucatán. Hali ya hewa iliyotulia katika makaburi haya inasaidia kwa kuwa kwa dakika chache athari inayojitokeza hutoweka wakati wa kulitembelea eneo hili mara ya kwanza. Tangu kati kati mwa mwezi Oktoba ndugu wa wapendwa waliofariki wamekuwa wakija kusafisha mifupa ya wafu wao na kuiweka tayari kwa tarehe 31 Oktoba na Novemba mosi, siku ambazo watoto na watu wazima wanaminiwa kurejea.
Familia huzungumza kwa sauti za chini wakiendelea kusafisha, wengine huweka maua na mishumaa na kupamba na nguo zenye michoro ya kupendeza na maua na majina ya wafu ambapo mifupa misafi itawekwa na kuruhusu kuondolewa zile zilizotumika mwaka uliotangulia.
"Kwa kusafisha ni kama wameoshwa na kwa nguo mpya ni kama wanabadilishwa nguo zao, kwa sababu karibu wanakuja kutembea na hivyo lazima waandaliwe. Mishumaa huwashwa ndio wapate kuona njia na kurudi nasi," anasema Ricardo Yam, anayefanya kazi ya kupaka rangi na mbaye anasafisha mifupa ya mmoja wa pacha mwenzake kila mwaka, baada ya kufariki miaka 28 iliyopita
Baadhi ya majirani hata hivyo ambao hupata ugumu wa kusafisha na kutunza mifupa ya jamaa zao kwa hivyo wanaomba msaada wa watu kama Venancio Tuz, mchimba kaburi katika makaburi hayo. Kwa haraka Don Venanchio kwa ustadi huosha mifupa ya wale humuomba afanye hivyo kwa chini ya dakika 15.
Mmoja baada ya mwingine huondoa vumbi kutoka kwa kila mfupa na kurudisha kwa masanduku yao kwa nguo mpya.
"Mpangilio wa kusafisha ni kuanzia chini kwenda juu. Ndio sababu mbavu huwekwa pande za sanduku, kisha mifupa ya miguu na mikono, na cha mwisho ni fuvu la kichwa linalowekwa juu. Unavyoona nywele hazipotei," anaiambia BBC.
Mchimba makaburi huyu anasema mifupa ya mtu aliyefariki ni lazima ipite miaka mitatu kabla ya mifupa yake ipate kusafishwa, kwa kuwa mwili wake utakuwa umeoza. Elewa kuwa kazi yako haimfai kila mtu. Anasema kuifanya ilimgharimu mara ya kwanza lakini sasa ameizoea baada ya miaka 20 ya kuifanya kazi hii. Wakati wa siku kama hizi anaweza kusafisha hadi miili ya watu 15 kwa siku. Malipo yake ni dola 1.5 kw amwili mmoja.
Mbele yake raia wawili wa kigeni wanatazama tambiko hilo huku wakirekodi kwenye simu zao. Kuna maeneo mengine yenye utamaduni sawa na huu, lakini Pomuch ndio huvutia watalii wengi.
Hatma ya utamaduni huu
Moja ya miili inayosafishwa na Don Venancio ni ya ndugu ya Carmen Naal.
"Anasema mumuwe kawaida hushugulikia hilo lakini mwaka huu aliamua kumuomba mchimba kaburi kusadia muda mfupi ulisalia kabla ya Novemba mosi. Pia mwaka huu mifupa imekuwa michafu kuliko kawaida kwa sababu mwaka uliopita hatukusafisha kutokana na janga la corona na pia mama yangu alifariki. Kwa hivyo hatungekosa kusafisha mwaka huu," Anasema kwa tabasamu.
Jirani huyu wa makaburi ya Pomuch. Ligia anazungumza kwa shauku kuhusu utamaduni huu ambao anajivunia. Kwa kusafisha mifupa ni wakati muafaka wenye hisia, unahisi ni kama unamkumbatia jamaa yako, tena kwa upendo.
Ziara katika makaburi haya pia zinaadhimishwa kwa shangwe na rangi nzuri zinazopakwa na kusafishwa ni kama nyumba inayorembeshwa, Ni kama wafu wamehama na sasa unawatembelea, anasema Naal.
Ana matumaini kuwa utamaduni huu hautatoweka na vizazi vipya na kusema kuwa wamewashauri watoto wake waandelee nayo kwake mara atakapofariki. Mmoja wao ni Maria Jose binti anayeandamana na mama yake na anayemuhakikishia kuwa utamaduni huo utandelea wakati hatapokuwepo.
"Tunaongea nao, ni kama tuko nao. Mwili wake ulikufa lakini mtu bado yuko nasi na siku hizi ni za kuwakumbuka. Ndio sababu wazazi wanawafunza watoto wao utamaduni huu, ninamuambia binti huyu: Huyu ni dada yako, yuko hapa umri wa miaka 30 na ni kama jana tu," anasema huku akizuia machozi.
Wale walio kwenye makaburi haya wataendelea baada ya siku ya wafu na kuonyesha sehemu ya mafuvu kutoka kwa masanduku ishara kuwa wanatutazama.
"Ni hali kama hii mabapo watasubiri kwa mieizi 12 kusafishwa na wapendwa wao. Na ndipo sasa ninaamini wafu wa Pomuch hawafi hadi tutakapo wasahau. Ndio sababu utamaduni huu ni umuhimu," anasema Pool.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.