Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, imepanga kukamilisha Jengo la ghorofa tisa ndani ya miezi 24 ambalo litakuwa na uwezo wakuchukua watumishi 400 kwa awamu ya kwanza.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt.Dorothy Gwajima wakati wa Hafla ya kutiana saini Mkataba wa ujenzi wa eneo la ujenzi katika eneo la Mtumba, mji wa Serikali.
Dkt. Gwajima amesema Makubaliano baina ya Wizara na Mkandarasi Nandhra, yamekuja mara baada ya Serikali ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kutoa fedha kiasi cha bilioni 23 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo hilo la Wizara ambalo litajumlisha Idara kuu Afya na Idara Kuu Maendeleo ya Jamii na kwamba”ni imani mradi utaanza kwa wakati na kukamilika ndani ya miezi 24 kama ilivyopangwa”. Alisema
“Hatutegemei kipindi cha Miezi 24, kipite kama maelekezo ya Serikali yalivyotaka halafu kazi iwe haijakamilika, ni Imani yetu Mkandarasi atakuwa na Mpango kazi utakao ainisha kila siku nini kitakuwa kinafanyika” Amesema Waziri Gwajima.
Dkt. Gwajima ameitaka Idara ya Tathmini na Ufatiliaji ndani ya Wizara kuto waachia kazi Mkandarasi na kukaa pembeni badala yake waweke kadi ya maendeleo (Score card) ya ujenzi na iwe inakaguliwa kila jumatatu ili kubaini maendeleo ya ujenzi, huku akihimiza Viongozi wa Wizara kufanyia Vikao vyao eneo la ujenzi (Site meetings).
Kwa Upande wao Wakala wa Ujenzi Nchini (TBA), ambaye ni Mkandarasi Mshauri, amemhakikishia Mhe. Waziri na Ujumbe wake kuwa, Mkandasi huyo, watamsimia ili kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo ndani ya kipindi ambacho kimepangwa au chini ya hapo, huku akisema Ana Imani na Mkandarasi Nandhra kutokana uzoefu wake.
“Mhe.Waziri Mkandarasi aliyepewa jukumu hili, anafahamika kwa sifa yake ya kuwa Mkandarasi daraja la kwanza, tunaimani kabisa, kazi hii ataikamilisha kwa wakati kama ilivyopangwa” Alisema Msanifu Majengo Wencelaus Kizaba kutoka TBA, na kuongeza kuwa, tayari taasisi hiyo imepeleka Wataalam 17 katika eneo hilo la mtumba ambalo kuna miradi mikubwa wa ujezi wa Ofisi za Wizara.
Naye Mkandarasi Iqbal Singn, akizungumza kwa niaba ya Kampuni ya Nandhra Engineering and Constructions, alisema wanashukuru kwakuaminiwa na Serikali lakini wao kama kampuni watahakikisha wanazingatia makubaliano ya Mkataba na kukamilisha kazi kwa wakati.
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, imesaini Mkataba na Mkandarsi Nandhra wa Mjini Morogoro, ambapo hafla hiyo imehudhuriwa pia na Makatibu Wakuu wa Wizara, Prof. Abel Makubi wa Afya Kuu na Dkt. James Jingu, Katibu Mkuu, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.