ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 2, 2021

SIRI YA BEYA KUSHIKA NAFASI TATU DARASA LA SABA HII HAPA.

 


Siku chache baada ya baraza la mitihani nchini, (Nacte) kutangaza matokeo ya darasa la saba, huku Mkoa wa Mbeya ukishika nafasi ya tatu kitaifa kwa ufaulu, Mkuu wa Mkoa huo, Juma Homera ameeleza siri ya mafanikio hayo.

Mbeya ilishika nafasi ya tatu bora kitaifa katika matokeo hayo yaliyotangazwa hivi karibuni, ikiachwa na kinara Dar es Salaam na Iringa iliyoshika nafasi ya pili.

Akizungumza leo Novemba 1 wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi kwa Waandishi wa Habari mkoani hapa, Homera amesema kujituma na kuchapa kazi ndio siri ya kufanikiwa.

Amesema alipowasili mkoani hapa alikutana na walimu ambapo miongoni mwa maazimio ilikuwa ni kuwaheshimu, kuwajali na kuthamini kazi za walimu.

"Nafikiri kikao cha mwisho na walimu hapa ukumbini, tuliazimia mambo mbalimbali lakini kubwa ni kuwaheshimu na kuwajali watu hawa, leo Mbeya tunapata matokeo mazuri" amesema Homera.

Hata hivyo Mkuu huyo amesema licha ya kuachwa na Dar es Salaam,lakini idadi ya shule zilizopo Mbeya ni nyingi kuliko Dar es Salaam zikiwa ni 738.

Kwa upande wake mmiliki wa shule za Paradise Mission, Ndele Mwansele amesema kutokana na mazingira mazuri ndicho kilichomsukuma kufanya uwekezaji wa Elimu mkoani humo.

Amesema kuwa sababu ambazo anaona zimechangia ni kujitambua kwa kurekebisha mapungufu kabla ikiwa ni Miundombinu na kuwasaidia wanafunzi walio kwenye mazingira magumu.

"Nimeamua kuwekeza Mbeya kielemu, lakini tumefanikiwa kutokana na kuboresha miundombinu, hadi sasa nimewasaidia wanafunzi 500 ambao wanaendelea na masomo wengine wapo makazini, nafanya hivi kwa kuamini katika Elimu kwani ndio imenitoa" amesema Mwansele

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.