ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 19, 2018

DIDDY ASEMA MAZITO BAADA YA KIFO CHA MKEWE.

Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani na mfanyabishara mwenye mkwanja mrefu zaidi kwa wasanii wa Marekani, Sean Combs maarufu kama Diddy, hatimaye amevunja ukimya na kusema machache baada ya kifo cha mama watoto wake Kim Porter.

Kwenye ukurasa wake wa twitter, Diddy ameandika ujumbe akisema kwamba kwa siku 3 mfululizo alikuwa akijaribu kuamka katika ndoto mbaya aliyokuwa nayo, kwani alikuwa hajui nini cha kufanya, lakini sasa atajaribu kuelezea mahusiano yao yasiyoelezeka.

“Kwa siku tatu zilizopita nilikuwa nikijaribu kuamka kutoka kwenye ndoto mbaya, lakini nimeshindwa, sijui nitafanya nini bila wewe baby, nakumiss sana. Leo naenda kutoa heshima, naenda kujaribu kutafuta maneno ya kuelezea mahusiano yetu yasiyoelezeka”, aliandika Diddy.


Diddy aliendelea kwa kuandika, "Tulikuwa ni zaidi ya marafiki wa karibu, zaidi ya soul mate, tulikuwa zaidi ya ujinga mwengine, na nakumiss sana."

Ijumaa ya Wiki iliyopita Diddy alipata msiba mkubwa wa kufiwa na mama watoto wake, mwanamitindo na muigizaji Kim Porter, ambaye aliugua kwa muda mfupi sana.

Kim Porter ameacha watoto wanne,  watatu kati yao ambao ni Christian, Dlila, na Jessie amezaa na Didy, huku mmoja anayejulikana kwa jina la Quincy, alimzaa kabla ya kukutana na  Diddy, lakini Diddy 'alimuadopt'.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.